Jana siku ya jumapili Dec 29, 2013 ndio kulifanyika hitma ya Marehemu Mohammed Omar Ghaza aliyetutoka tarehe 23 mwezi wa December waka 2013.
Hitma ilifanyika Durham, NC .
Nassor , Eddy, Yafidh, Amani na wengineo wakitia Fatha kabla ya kuomba Dua.
Watanzania na marafiki zao wakijumuika pamoja kwenye hitma ya Mohammed Ghaza iliyofanyika Durham, North Carolina nchini Marekani Jumapili ya Dec 29, 2013.
Hitma ya marehemu Mohammed Ghaza aliyefariki kwa ajali ya gari mapema asubuhi ya Dec 23, 2013 kwenye makutano ya Martin Luther King Jr. Boulevard na Elm Eugene Street. Marehemu alikuwa na mchumba wake Christa aliyekuwa akiendesha Ford Focus ya mwaka 2001 akielekea mashariki na marehemu akiwa abiria gari ilipoteza muelekeo na kutoka nje ya barabara na iliporudi ikagongwa na trela ya trekta iliyokua ikiendeshwa na Rodney Morris Marehemu alikimbizwa hospitali ya Moses Cone na kufariki baadae kutokana na majereha aliyopata. Christa anaendelea vizuri.
Watanzania na marafiki zao wakijumuika pamoja kwenye hitma ya Mohammed Omar Ghaza iliyofanyika Durham, North Carolina nchini Marekani siku ya Jumapili Dec 29, 2013.
Watanzania na marafiki zao wakijumuika pamoja kwenye hitma ya Mohammed Omar Ghaza iliyofanyika Durham, North Carolina.
wakati wa kupata makulaji
Ndugu jamaa na marafiki wakipata sunna ya chakula.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. We Mushobozi mbona usemi kuwa uko NC?. kimyakimya mzee

    Haya bwana ukirudi Bongo nitafute twende kaloleni.

    ReplyDelete
  2. Wow namwona ndugu yangu Teddy wa Arusha.

    ReplyDelete
  3. Hitma za Marekani kwa Mahanjumati ni kama miaka ileee huku Bongo, unakuta Shaba kadhaa zinashuka.

    Lakini sasa Bongo Hitma mnakuta mnaishia Kahawa, Juisi na Biskuti!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...