Globu ya Jamii inatoa pongezi kwa wahariri wa magazeti ya Rai na Mwananchi kwa kuwa magazeti pekee nchini yaliyoweza kutoa habari za kifo cha Mzee Nelson Mandela ambaye alifariki dunia saa 3 na dakika 10 usiku wa kuamkia leo.
Magazeti haya sio tu yameonesha ni vipi mhariri anatakiwa awe, bali pia juhudi zao hizo ni kengele ya kuamka kwa vyombo vingine vya habari ambavyo ukiviuliza kwa nini wameikosa stori hii kubwa kuliko zote duniani kwa sasa watakwambia wao humaliza kazi mapema na isingekuwa rahisi kuchapa upya gazeti kwa habari moja ya Mandela!
MAnaging Director= Tido Mhando, Kama sijakosea.
ReplyDeleteHe is from diaspora........haya sasa wadau changieni mawazo yenu.
Mdau UK.
Yaleyale alio ongea Mwakyembe kuhusiana na TRA kwenda kuchapa usingizi wakati shughuli za bandari zikioperate 24/7.Tuache kufanya kazi kwa mazoea,.
ReplyDeleteMdau udayaspora hapo unaingiaje!! Vyombo vingine vya habari havina watu diyaspora?
ReplyDeleteMdau wa kwanza anachomaanisha ni work ethics au kujali kazi yako kwa kujua nini mteja wako anataka!!
ReplyDeleteKama haijaeleweka, basi WaTZ tuna safari ndeeeeeefu, na kufungia Labour Market kwa wageni kutafanya hata private sector ififie kwa sababu ya kukosa wazawa wenye sifa za kazi!!
Lazima tukubali, TZ kuna tatizo kubwa la nguvukazi, labda ndio maana wenye shughuli binafsi wanafidiwa kwa udhaifu huu kupitia punguzo la kodi (in EA ni lowest average), huku wafanyakazi wakiadhibiwa kufidia hiyo tofauti!
Kumbe unaweza kujifunza hali ya jamii kwenye matukio yanayoonekana ya kawaida ya kila siku.
RIP Madiba, thanks Rai na Mwananchi!!
Kama wapo Kutoka diaspora basi sio ngazi ya juu....na Kama wapo ngazi ya juu basi wamebweteka na uchapakazi walioukuta hapo bongo.
ReplyDeleteCongrats Mwananchi na Rai, Niliona hili na nika-comment lakini nikagundua kuwa wabongo wengi hawajagundua hiyo tofauti iliyofanywa na hayo magazeti. Magazeti yamejaaa Zitto, Chadema, Lowasa basi. Watanzania tumechoka na siasa na kelele zake tunahitaji vitu vya maana zaidi.
ReplyDelete