Katika maisha ya binadamu Mwenyezi Mungu hutoa watu, wachache sana, wanaojitolea na kujitoa mhanga na kubadili mkondo wa historia na maisha ya wengi.
Nelson Rolihlahla Mandela hakika alikuwa ni zawadi ya Rabuka kwetu. Tusherehekee maisha yake kwa kufuata,tena kwa dhati kabisa, yale yote aliyoamini, yale yote aliyopigania, na tuyatekeleze kwa vitendo. 
Mandela alikuwa Mtu,
Mtu katika watu, Mtu wa watu.
Kwaheri Mandela.
Hakika hutarudi.
Hakika tutakufuata.
Msalimie Mwalimu.
Maulana awarehemu.
Mpumzike katika Mtaa wa Amani ya Milele.
 
-Mark James Mwandosya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...