Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknologia, Mhe. January Makamba
Jumuiya ya Watanzania DMV inapenda kuwakaribisha Watanzania wote siku ya Jumapili Desemba 8, 2013 Mhe. January Makamba atakapoongea na wana DMV na kutakuwa na kipindi cha maswali na majibu. mkutano huo utafanyikia Mirage Hall anuani ni 1401 university Blvd, Hyattsville, MD 20783 pia Bw. Mayingu na msafara mzima wa kutoka mfuko wa pensheni watakuwepo kuelezea habari njema kutokana na mfuko huo.
Muda ni kuanzia saa 11 jioni na tunaomba tuzingatie muda. Vimiminika vyepesi na Vitafunwa vitakuwepo Karibuni sana na ukupata ujumbe huu tafadhali mtaarifu mwenzako
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...