Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wakazi wa Mbeya mjini, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana jioni katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa huo, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.
 Katibu NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akihutubia maelfu ya wananchi wa Mbeya, katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana jioni katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa huo, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.

 Sehemu ya Wakazi wa jiji la Mbeya Mjini wakishangilia jambo wakati Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye alipokuwa akihutubia,katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana  jioni katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yao katika mkoa huo.
 Pichani kati ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakiwapungia mikono wakazi wa jiji la Mbeya waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM,uliofanyika katika uwanja wa Rwanda Nzovwe,nyuma ni Katibu wa NEC,Siasa na mahusiano ya Kimataifa Dkt.Asharose Migiro.
  Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa kwenye Bajaj huku akiwapungia mkono baadhi ya Wananchi na Wanachama wa CCM,waliokuwa wamejipanga barabarani kushuhudia tukio hilo la aina yake wakati Ndugu Kinana akiwa ameambatana na msululu wa Bajaji akielekea kwenye mkutano wa hadhara,anaekimbia pichani kulia ni Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye .
 Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwapungia mkono baadhi ya Wananchi na Wanachama wa CCM,waliokuwa wamejipanga barabarani kushuhudia tukio hilo la aina yake wakati Ndugu Kinana akiwa ameambatana na msululu wa Bajaji akielekea kwenye mkutano wa hadhara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hawa makamanda ni tishio kwa chadema

    ReplyDelete
  2. Well said Chief, hao makamanda kwa speed hii nadhani M4C lazima ibadilishe "gea" vinginevyo ........

    ReplyDelete
  3. CCM pamoja na yote kuna walio na moyo na uchungu na nchi yetu...mama Migiro pamoja na kula kuku zote UN lakini amedhihirisha ni mpambanaji wa ukweli..nafikiri wana zaidi ya mwezi sasa wako kanda ya kusini wanapambana...CDM mjipange upya huu ni moto mkali haswa!!!!Big up hii Timu ya majembe ya ukweli.
    mdau wa Norway.

    ReplyDelete
  4. NIMEWAKUBALI KWA KUJITAHIDI KUJISHUSHA KATIKA NGAZI YA MWANANCHI WA KAWAIDA. KAMA MIOYO YA VIONGOZI WENGI INGEKUWA HIVI KWELI TUNGEKUWA NA MATUMAINI. MAMA MIGIRO HONGERA KWANI UMEONYESHA UZALENDO WA KIPINDI CHA NYERERE. ILA NAOMBA ISIWE NGUVU YA SODA NA MBIO ZA UCHAGUZI TU, ITOKE MOYONI NA DAMUNI.

    ReplyDelete
  5. Mama Migiro mi namheshimu sana kwa kweli ni mpambanaji nimemfuatilia sana amefanya mambo makubwa huu mchaka mchaka si kawaida ila mama kahimili vishindo.

    ReplyDelete
  6. Kwa siku za karibuni matukio kama haya CCM tuliyazoea nyakati za uchaguzi, ila si haba kipindi hiki kazi mmeifanya, kuwa karibu na wananchi. Hongereni kwa kutengeza mambo ya chama chenu!

    sesophy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...