Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limetembelea kituo cha matumaini cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu URSOLINE SISTERS Kilichopo eneo la Miyuji Manispaa ya Dodoma na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo Mchele Kg. 50, Maharage Kg. 50, Sabuni Boksi 2, Mafuta ya kupikia Lt. 20, Pamoja na chumvi.

Akiongea na watoto hao katika kituo hicho Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SUZAN KAGANDA – ACP amesema pamoja na jukumu la ulinzi na usalama wa watu na mali zao, lakini pia ni jukumu la Polisi kuwatembelea watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu,pamoja na kutoa elimu ya usalama wetu kwanza na usalama barabarani kwa kuongea nao na kuwaelekeza majukumu ya ulinzi na usalama.

Kamishna msaidizi wa Polisi KAGANDA aliwapongeza watoto wanne ambao wamefaulu Darasa la saba kwa kuwapatia zawadi za Madaftari 36, Mikebe 4, Peni na Penseli Boksi 4 na kusema kuwa wameonyesha moyo kwa walezi wao katika kituo hicho.

Kwa upande wake Sista ANITHA KASANGA kwa niaba ya masista wenzake ambao wanajukumu la kuwalea watoto hao amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kuthamini kazi inayofanywa na kituo hicho na kuwaunga mkono kwa kutoa msaada kwa watoto hao na kuonyesha moyo wa ukarimu.

Aidha Sista KASANGA alisema kituo hiki kipo chini ya Kanisa katoliki na kilianzishwa mwaka 1995 kikiwa na jumla ya watoto 6 ambapo mpaka leo hii kina jumla ya watoto 53, kwa hapa nchini Tanzania makao makuu ya kituo yapo Mkoani Singida, lakini makoa makuu yake yanapatikana nchini Poland na mpaka sasa kituo hiki kina jumla ya matawi 27 hapa nchini.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi IVONIA akitoa elimu ya usalama barabarani kwa watoto hao.
Baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali wawakilishi toka Jeshi la Polisi walipata chakula mchna na watoto hao waishio katika mazingira magumu.
Kaimu Kamanda Mkoa wa Dodoma akikabidhi vifaa mbalimbali kwa Sista ANITHA KASANGA ambaye ni mlezi wa watoto hao.
Kamishna msaidizi wa polisi SUZAN KAGANDA akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha Miyuji - URSOLINE SISTERS.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Bravo,
    If coppers are serving people beyond just dealing with criminals and other notorious things we hear everyday, they will create a very meaningful relationship with the society.This will also restore faith in cops to our society.

    ReplyDelete
  2. Hongera jeshi la polisi Dodoma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...