Na Pamela Mollel,Arusha
KAMPUNI ya Megatrade Ivestment kupitia kinywaji chake cha K-vant Gin imetoa misaada ya vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwaajili ya sikukuu ya krismasi na mwaka mpya katika kituo cha New Paradise kilichopo kata ya sokoni 1 jijini Arusha
Akikabidhi msaada huo juzi kituoni hapo Meneja mauzo na masoko Goodluck Kway wa kampuni ya hiyo kupitia kinywaji chake cha K-vant Gin alisema utowaji wa misaada kwa makundi maalum yenye uhitaji ni utaratibu wao wa kurudisha faida waliopata kwa mwaka mzima kwa jamii
Alisema msaada huo walioutoa umegharimu kiasi cha shilingili Milioni moja, ambapo watoto hao watasherehekea sikukuu kama watoto wengine, huku akitoa rai kwa makampuni kujitokeza kuwasadia watu wenye uhitaji wa namna mbalimbali.
Misaada iliyokabidhiwa kituoni hapo ni pamoja na sukari,mafuta ya kula,mchele,katoni za soda,sabuni,kalamu,madaftari,unga wa ugali,unga wa ngano na maziwa.Mlezi mkuu wa kituo hicho Christopher Kaaya alisema kampuni hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao na amewaomba waendelee na moyo huo wa kuwasaidia
“Mungu awazidishie sana kwa sababu wamekuwa watu wa karibu kwetu hata siku ya kwanza walituchangia katika ujenzi wa jengo hili na pia kila mwaka lazima watuletee zawadi za chrismasi na mwaka mpya”alisema Kaaya
Kituo hicho kinajumla ya watoto 24 wasichana wakiwa 14 na wavulana 10 ambapo idadi imeongezeka ukilinganisha na mwaka jana watoto walikuwa 20 tu kituoni hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...