Chuo cha Diplomasia Dar es salaam, katika kuendeleza wito na wajibu wa kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu, kati ya  tarehe 25 na 29 Novemba 2013 kilifanya kozi fupi ya ITIFAKI NA MAHUSIANO YA UMMA (PROTOCOL AND PUBLIC RELATION) Chuoni Kurasini, Dar es salaam
Washiriki  walitoka maeneo mbali mbali katika sekta binafsi na mabenki kama CRDB Plc na Sekta ya Umma, Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa J.K.Nyerere(JNIA), Mkuu wa Wilaya ya Temeka, Mhe. Sophia Mjema na kadhalika.
 Wawezeshaji wa Mafunzo haya ya muda mfupi kawaida huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea sana katika mambo ya Diplomasia hivyo kuwapa washiriki uzoefu na kesi halisi zilizowahi kutokea katika eneo husika la mafunzo ili kuwajengea uwezo na waweze kwenda kufanyia kazi moja kwa moja mafunzo na utaalam walioupata. 
 Akifunga mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi, Bwana, Juma M. Kanuwa akisisitiza  umuhimu wa utaalam wa mambo ya Itifaki na Mahusiano ya Umma, katika sehemu za kazi, alisema kuwa mafunzo hayo  yatarudiwa tena mnamo tarehe 16th – 20th Desemba 2013 hapo Chuo cha Diplomasia ili wale wote walioshindwa kuhudhuria hapo awali wajitokeze  kwa wingi na kupata mafunzo hayo toka kwa mabalozi na wataalam waliobobea na wenye uzoefu wa miaka mingi.
 Washiriki wakimsikiliza na kufuatilia kwa makini mafunzo ya Itifaki (Protocol) toka kwa mmoja wa wawezeshaji Balozi C. A. Sanga ( hayupo pichani)
Mkuu wa Wilaya ya Temeka, Mhe. Sophia Mjema akishiriki katika moja ya mijadala
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi wa  Taaluma, Utafiti na Ushauri, Dr. Wetengere Kitojo (aliyekaa katikati mwenye shati la mikono mirefu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...