MZEE HUDSON CHACHA RYOBA
(08/12/1933 – 15/12/2007)

Baba yetu mpenzi ni miaka sita saa imetimia tangu ulivyotuacha kimya bila ya kuongea. Uliweza kuona kila kilichokuwa kinatendeka lakini kwa maumivu makali uliyokuwa nayo hukuweza kuzungumza. Ni huzuni kubwa sana kutengana nawe mpenzi wetu, lakini tunajua kwamba ipo siku itafika tutakuwa pamoja nawe mbinguni kwa Mungu.

Baba urithi mkubwa wa maneno yako ya busara na hekima ndiyo imekuwa nguzo kubwa katika maisha yetu ya kila siku. Unakumbukwa sana na wake zako na watoto wako Marwa, Leah, Debora, Bhoke, Taifa, Muniko, Mariba, Nyangi, Samwel, Wankyo na Stan.

Pia bila kuwasahau wadogo zalo, marafiki zako, watani na wote waliokufahamu . Tunakosa vichekesho vyako kwani ulikuwa ni changamamoto ya furaha pale palipo kuwa na huzuni.

Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi.
Amen. 
 (Revelation 15:4) (Psalms 100)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mtani wetu mzee Chacha, hatutamsahau kamwe. Nakumbuka akianza kutania wahaya wote ni kenge pale mtaani urambo. Tutakukumbuka daima sie majirani zako. Mungu awafariji familia ya mzee Chacha.

    ReplyDelete
  2. Mzee Chacha, sitamsahau.Nilikuwa pale Urambo st (Hostel ya Tambaza sec 1986-1988).Nilimfahamu zaidi kwa kupitia jirani yake pale Urambo ambaye ni rafiki yangu (Prudence K.)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...