MZEE HUDSON CHACHA RYOBA
(08/12/1933 – 15/12/2007)
Baba yetu mpenzi ni miaka sita saa imetimia tangu ulivyotuacha kimya bila ya kuongea. Uliweza kuona kila kilichokuwa kinatendeka lakini kwa maumivu makali uliyokuwa nayo hukuweza kuzungumza. Ni huzuni kubwa sana kutengana nawe mpenzi wetu, lakini tunajua kwamba ipo siku itafika tutakuwa pamoja nawe mbinguni kwa Mungu.
Baba urithi mkubwa wa maneno yako ya busara na hekima ndiyo imekuwa nguzo kubwa katika maisha yetu ya kila siku. Unakumbukwa sana na wake zako na watoto wako Marwa, Leah, Debora, Bhoke, Taifa, Muniko, Mariba, Nyangi, Samwel, Wankyo na Stan.
Pia bila kuwasahau wadogo zalo, marafiki zako, watani na wote waliokufahamu . Tunakosa vichekesho vyako kwani ulikuwa ni changamamoto ya furaha pale palipo kuwa na huzuni.
Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi.
Amen.
(Revelation 15:4) (Psalms 100)
Mtani wetu mzee Chacha, hatutamsahau kamwe. Nakumbuka akianza kutania wahaya wote ni kenge pale mtaani urambo. Tutakukumbuka daima sie majirani zako. Mungu awafariji familia ya mzee Chacha.
ReplyDeleteMzee Chacha, sitamsahau.Nilikuwa pale Urambo st (Hostel ya Tambaza sec 1986-1988).Nilimfahamu zaidi kwa kupitia jirani yake pale Urambo ambaye ni rafiki yangu (Prudence K.)
ReplyDelete