MAREHEMU MWL JOHN .C. KAYUZA
Leo 02/12/2013 Umetimiza miaka mitatu tangu ulipoitwa na Baba yetuwa mbinguni . Siku isiyoweza kusahulika katika maisha yetu.
Unakumbukwa sana mkeo Edna, watoto wako Mrs. Mwaisupule (Josephine) Masauko, Hellen na Simon, wajukuu zako Gave na Edna , Mkwe wako Japheth Mwaisupule.
Kaka yako Mathew na familia yake, Wadogo zako Joseh na familia yake, Charles na familia yake, Jerome. Dada zako Mrs. Chimwemwe na familia yake, Tayamika, Flora, Mrs. Nkoma na familia yake, Mrs. Mandawa na familia yake. Unakumbukwa na binamu yako Jaji Barnabas Samatta na familia yake. Unakumbukwa na Familia ya Mbiza, Familia ya Poyo, Familia ya Chikoko.
Unakumbukwa na Shemeji zako familia ya Muya, familia ya Ntemo, familia ya Chilimo, familia ya Chilewa.
Unakumbukwa pia na ndugu wote, jamaa, marafiki na wanafunzi wako wote popote walipo.
Ulikuwa na moyo wa upendo na wakujituma zawadi uliyozawadiwa na Baba wa yetu wa mbinguni.
Tulikupenda sana lakini mungu alikupenda zaidi. Roho ya milele umpe Ee Baba na mwanga wa milele umwangazie. astarehe kwa amani.
Misa ya kumbukumbu itafanyika katika kanisa la Watakatifu wote Anglicani Temeke.
Tarehe 07/12/2013 saa mbili asubuhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...