Kilio cha furaha kwa Moureen Julius.
Wow.....!!!...Hongera Mwanangu.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akikabidhi kitita cha Shilingi Milioni tano za Kitanzania kwa Supa Staa wa Shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Moureen Julius (12). Wanaoshuhudia tukio hilo ni baba mzazi wa Moureen pamoja naAfisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko ambao ndio waandaji wa shindano hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko, akiwa ameongozana na Supa Staa wa Shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Moureen Julius (12) huku nyuma yao wakiwa na ulinzi mkali kuelekea kuzungumza na waandishi wa habari.
Mniite mshamba mjima lakini nimeangalia huyo binti alivyokuwa anacheza wala sijapendezewa nako. Nazungumza kama Mama mwenye Binti wa umri sawa na huyo, kucheza kwake ni kwa kichochezi na sio kumlinda huko ni kumfungulia milango ya kuandamwa labda kama angekuwa na miaka 18 nako ingekuwa mbinde. Nasema kwa roho safi mashindano ya watoto wadogo yazingatie maadili. Nisinge mpa ushindi kwa kipengele cha maadili tu.Yuke mtoto aliyeimba na kucheza kwa kujinyonganyonga kwangu mimi angekuwa mshindi. Tuthamini watoto wakike
ReplyDelete