Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela leo amewaaga
Wakuu wa Idara na Mameneja wa Majengo mbalimbali waliomaliza muda wao katika nafasi za
Uongozi tangu walipochaguliwa kushika nyadhifa hizo Januari 2010 hadi Disemba 2013.
Akitoa neno kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Njelekela
amewashukuru kwa kumpa ushirikiano mkubwa tangu alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji
Novemba Mosi, 2011 na kwamba wamekuwa bega kwa bega katika kutekeleza majukumu
mazito ya kutoa huduma kwa wananchi.
“Nimejifunza mengi kutoka kwenu kama viongozi wenzangu ambao tumesimamia
utendaji katika maeneo yenu na ninafarijika kwamba uzoefu mlionipa umenisaidia
sana kuijua Hospitali ya Taifa Muhimbili katika Nyanja mbalimbali za kiutendaji” alisema Dkt. Njelekela.
Nawaomba wale mtakaorudi katika nafasi hizo katika kipindi kijacho cha 2014 hadi 2016
tuendelee kushirikiana na wale ambao watajiunga na timu hii mpya basi nawaomba
muwape ushirikiano kwani kazi hii ni ya kupokezana kijiti, amesema Dkt. Njelekela.
Jumla ya Wakuu wa Idara 28 na Mameneja wa Majengo 15 wamemaliza muda wao
leo ambapo timu mpya ya wakuu hao inatarajiwa kuanza kazi mara moja ifikapo Januari 2014.
Kiutendaji, Hospitali ina Kurugenzi nane ambazo ni Kurugenzi ya Tiba, Kurugenzi ya Huduma za Upasuaji,
Kurugenzi ya Huduma za Tiba Shirikishi (Maabara, Radiolojia, Famasi), Kurugenzi ya Huduma za Uuguzi,
Kurugenzi ya Fedha na Mipango, Kurugenzi ya Utumishi, Kurugenzi ya Ufundi na Kurugenzi ya Tehama,
ambazo chini yake kuna idara 28 na Wakuu wa Majengo 15 pamoja na Vitengo mbalimbali zaidi ya 100.
Wakurugenzi wa Kurugenzi hizo bado hawajamaliza muda wao kwa kuwa nafasi zao zinatofautiana
kulingana na kila mmoja alivyoteuliwa. Fuatilia katika picha baadhi tu ya Wakuu wa Idara na
Mameneja wa Mjengo waliopewa vyeti vya kutambua utumishi wao;
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili katika picha ya pamoja baada ya kuwatunuku vyeti
Wakuu wa Idara, Mameneja wa Majengo waliomaliza muda wao katika nyadhifa hizo Januari 2010 hadi Disemba 2013.
Prof. Victor Mwafongo aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura akipokea cheti chake kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Njelekela.
Aliyekuwa Meneja wa Jengo la Wazazi Sista Amina Mwakuluzo akipokea cheti chake.
Dkt. Rachel Mhaville, aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Meno.
Kumbe huyu ndie njelekela............
ReplyDelete