Hii ni chupa ya moja ya pilipili kali kuliko zote duniani. Inatengenezwa nchini Rwanda na mfanyabiashara maarufu nchini humo aitwaye Sina Gerard. Alianza kufanya biashara ya kuoka mikate na kuiuza kwenye kiosk pembeni mwa barabara miaka takriban 25 iliyopita, akiwa na mfanyakazi mmoja tu. Hivi sasa yeye ni milionea mkubwa sana  anayeajiri mamia ya wafanyakazi pamoja na kuwapa biashara maelfu ya wakulima wadogo kwa kuwapa pembejeo na mbegu na kisha kununua mazao yao. 
Kwa hapa kwetu tunaweza kumfananisha na Bakhressa. Tunaileta taarifa hii hapa kufuatia ripoti yetu ya juzi kutoka wilayani Rungwe, ambako wakulima wanalalamika kwa kukosa soko la ndizi zao (BOFYA HAPA). Si vibaya wahusika wakaangalia njia za kuwapeleka watu hao wa Rungwe na kwingineko kwa Bwana Sina Gerard kupata msaada wa mawazo ya nini kifanyike. Kwani pamoja na pilipili yeye pia anasindika na kuuza bidhaa zitokanazo na ndizi pamoja na matunda mbalimbali. 
Kwa taarifa zake zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wow nilikuwaga naitumia hii na marafiki zangu kutoka Rwanda. Jamani stori ya huyu jamaa inatia moyo sana. Watanznaia tuna utajiri mwingi na tunabidi tujiweke vizuri kibiashara. Tutawaachia wawekezaji wa nje biashara mpaka lini???

    ReplyDelete
  2. he! hii pilipili hata mimi nilisha itumia, kuna rafiki yangu kutoka Rwanda aliwahi kunipatia vichupa viwili, kumbe inahistoria ya namna hii.

    Ngoja na mimi niingie kwenye ujasiriamili, mambo ya kusema mtaji mdogo sitaki tena kuyasikia, nitaanza tu na nilicho nacho.Lol.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...