Nyota mahiri wa nyimbo za injili,ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Facebook na Shikilia Pindo la Yesu,Rose Muhando akiimba huku akiwa amezungukwa na washabiki na wapenzi wa nyimbo za injili ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid,jana jijini Arusha.Rose Muhando pia aliwaasa wakazi wa jiji hilo na kwingineko kuitunza amani ya nchi yetu tulionayo,kuonesha upendo na mshkamanno miongoni mwetu kuhakikisha nchi yetu inabaki kuwa salana na yenye amani daima dumu.
Tamasha hilo linaloandaliwa na kampuni ya Msama Promotions Ltd,liko kwenye mwendelezo wa uzinduzi wa tamasha la Krismasi kwa mikoa mitano kuelekea kuupokea Mwaka mpya,ambapo siku ya mwaka mpya tamasha hilo litafanyika mkoani Dodoma na kuwahusisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili ndani na nje ya nchi.
Sehemu
ya wapenzi wa nyimbo za injili wakiwa kwenye tamasha hilo huku wakiwa
na hisia ya kuguswa mno kupitia nyimbo mbalimbali zilizokuwa zikiimbwa
na waimbaji mbalimbali waliokuwepo kwenye tamasha hilo liliofanyika
ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid hapo jana.
Mmoja wa waimbaji mahiri wa nyimbo za injili,Bone Mwaitege akiimba huku akiwa amezungukwa na mashabiki wake.
Pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions inayyoandaa matamasha ya Pasaka na hili la Krismasi,Bwa.Alex Msama akiwashukuru wakazi wa jiji la Arusha kwa kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo,aidha amewataka wakazii wa jiji hilo kuhakikisha wanadumisha amani na upendo walionayo miongoni mwao,ili kuifanya nchi yetu iendelee kujiwekea historia ya kulinda,kutunza,kudumisha na kuienzi amani yetu kwa nguvu zote.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...