Na Kiza Sungura
Taasisi ya Elimu Tanzania [TET]imedhamiria kuendelea kuboresha utendaji wake ili kuinua kiwango cha elimu nchini.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wataasisi hiyo Dr.Leonard Akwilapo wakati akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es Salaam.
Dr. Akwilapo alisema kuwa kwa kuzingatia mpango mkakati wamaendeleo wamiaka mitano (2011- 2016), taasisi hiyo inatarajia kufanya maboresho katika majukumu yake mbalimbali kwa lengo la kuleta tija katika sekta ya elimu nchini.
Akitaja mipango ya taasisi hiyo Dr. Akwilapo alifafanua kuwa ni pamoja na kufanya tahakiki ya mitaala katika ngazi zote, kuandaa vifaa vya kujifunzia nakufundishia vikiwemo vitabu, vifaa vya kielektroniki na vipindi vya redio na televisheni.
Aidha TET inatarajia kukamilisha andiko la Mwongozo wa Taifa wa Ukuzaji Mitaala, kufanya tathmini ya utekelezaji wa mitaala ya elimu ya awali hadi sekondari na kuendesha makongamano ya kitaifa na kimataifa kuhusu mitaala.
Pia Dr. Akwilapo aliongeza kuwa wana mpango wakujenga kituo cha kisasa cha mafunzo ya ukuzaji mitaala eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, kuandika sera ya utafiti na uelekezi wa kitaalam pamoja na kuendesha mafunzo elekezi kwa walimu na watekelezaji wa mitaala.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Ubunifu naUboreshaji Mitaala ya taasisi hiyo Bi Angela Katabaro alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita taasisi imeweza kuboresha mihtasari ya masomo 26 ya ualimu ngazi ya cheti kwa elimu ya awali na msingi.
Pia Bi Katabaro aliongeza kuwa taasisi hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI ilichapisha na kusambaza mihtasari na miongozo ya masomo yote ya shule za msingi.
Kwa upande waelimu ya sekondari taasisi iliweza kuboresha mihtasari 25 ya kufundishia kidato cha tano na sita na kuendesha mafunzo ya utekelezaji wa mtaala wa sekondari kwa walimu wa shule mbalimbali za sekondari hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...