Mashabiki wakifurahi burudani iliyokuwa ikitolewa juu ya steji.
Msanii
Nguli wa muziki wa kizazi kipya,Chege Chigunda a.k.a Mtoto wa Mama Said
akitumbuiza mbele ya mashabiki kibao waliofika kwenye tamasha la After
Skull Bash,lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi,Mikocheni jijini
Dar. Tamasha hilo limeratibiwa na Clouds FM kwa
kushirikiana na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time
Promotions Ltd.
DJ Mahiri kutoka Clouds FM,Dj Zero akifanya makamuzi ya nguvu ndani ya Mbalamwezi Beach,wakati wa tamasha la After Skull Bash likiendelea,Tamasha hilo limewakutanisha wanafunzi wa shule mbalimbali jioni ya leo.
Msanii wa muziki wa Kizazi kipya,ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga ya muziki wa bongofleva,Rich Mavoko akikamua vilivyo jioni ya leo kwenye tamasha la After Skull Bash,lililofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar.
Watangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu na Dj Fetty wakijadiliana jambo nyuma ya jukwaa.
Mashabiki kibao wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri jukwaani jioni ya leo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...