Kaimu Mhandisi wa Maji Manispaa ya Temeke, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Meckiline Haule (katikati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa gharama ya sh. mil. 35 katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Wanaoshuhudia ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Isabela Ipopo (kushoto),Mwakilishi wa Mauzo wa TBL, Allen Mwebuga (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Rumelius Bakilane.
Mwebuga wa TBL (kushoto) na Bakilane wakifujaza maji kwenye ndoo wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Rumelius Bakilane akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Kijiji cha Kibada, Diana Salvatory baada ya kampuni hiyo kukabidhi kisima cha maji katika Zahanati ya Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kisima hicho chenye uwezo wa kuhifadhi maji lita za ujazo 1,600 kwa saa uchimbaji umegharimu sh. mil 35 zilizotolewa msaada na TBL.
Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu akielezea mikakati ya TBL kusaidia miradi ya maji nchini ambapo kwa mwaka wafedha wa TBL tayari imetenga sh. mil. 450 kwa kazi hiyo.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...