Basi hapo wakisemwa ama hatua zikichukuliwa dhidi ya kuvunja sheria waziwazi namna hiyo wanakuja juu na kudai wanaonewa....Hapa ni pembezoni mwa barabara ya Nyerere (zamani Pugu Road) jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dares salaam. Na alama hii inamaanisha ni marufuku kupita ama kuegesha gari sehemu yote hiyo.....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Haguswi mtu hapa! Jaribu uone mmesahau eeenhe,wahusika wenyewe kimyaaaaaaaa.Wataishia kuweka mabango yasiyo na tija.

    ReplyDelete
  2. Kwa dereva aliyesomea udereva hapo hakuna aliyevunja sheria. Madereva hao walioegesha malori yao yaonyesha wamesoma na wanazielewa sheria na alama za barabarani. Alama hiyo ya kukataza inaonyesha katazo la malori yasiegeshe mbele ya alama hiyo, lakini nyuma yake inaruhusiwa kuegesha na ndivyo madereva hao wamefanya. Isitoshe hapo haionyeshi kuwa ni Tanzania, lakini kwa vile tumezoea kuona kosa la aina yoyote ni la kutupiwa Tanzania mtu kaona kitu hiki na kurusha hewani ili maporomoko ya kashifa kwa nchi yetu yaporomoke kwa viongozi wetu wa Tanzania. Kuweni Wazalendo na nchi yenu.
    _ Mr MHOJA - Sweden

    ReplyDelete
  3. Mr Mhoja, hi alama ni-malori hayaruhusiwi kuegesha au kupita?

    ReplyDelete
  4. Alama hiyo ni ya kuzuia malori aina hiyo kupita. Malori hayo hayaonekani kuipita alama hiyo, bali yanaonekana yameegeshwa nyuma ya alama hiyo, kitu ambacho alama hiyo haijakataza. Hata kama kungekuwa na makosa huwezi kuihukumu Tanzania kwa kila kosa linalotokea sehemu ambayo huna hakika kama ni Tanzania.
    - Mr MHOJA - Sweden

    ReplyDelete
  5. Mdau wa TokyoDecember 05, 2013

    Mhoja acha porojo..Hapo Tz Bongoland..Angalia vizuri namba za lori la upande wa kulia zinaonekana kabisa kuanza na T...na ndizo namba zinazotumika Tanzania sasa,hata herusfi zinazofuata baada ya namba pia zinaonyesha ni namba za magari za usajili Tanzania.Kama hapo sio Tanzania basi magari hayo ni ya Tanzania. Fanya uchunguzi kabla ya kukurupuka.Uzembe kwa madereva wetu ni kawaida,mimi nipo hapa Japan sijawahi kuona ajali ya gari mjini hata siku moja kwa miaka 3 sasa..Huko kwetu ajali ni kila baada ya dakika kadhaa tu.TUBADILIKE..!!

    ReplyDelete
  6. Bwana mhoja ni kati ya wale wale ambao sheria kwao haipaswi kuwagusa hivyo kufanya kila hila ikiwemo ya kupotosha ukweli ili muradi waendelee kufanya madudu yao kwa gharama ya umma. Sawa tumekuelewa endelea kufanya uharibifu usije ukagoma tena tukakosa kwenda krismas!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...