Watanzania ebu angalieni uhalibifu huu. Hili roli linalizimisha kupita kwenye daraja la mto Kilombero leo. Ukiangalia hapo juu Kushoto na kulia pamekatika!!! Na watu wote tuko hapa tumekwama tangu asubuhi TANROAD wako wapi? Na hii ni gharama ya nani? Jamani Watanzania!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hivi hapo ni nani mwenye kosa? Hivi kila kitu ni lazima viboko?

    ReplyDelete
  2. NYUMA YA LORI HILO LIMEANDIKWA (RISPECT elimu mbovu) RESPECT YAANI HESHIMU, SASA INABIDI SISI TUHESHIMU MAAMUZI YAKE!

    ReplyDelete
  3. Kwa mdau wa kwanza, Tanroad hayupo kila sehemu, ni wajibu wa wananchi mlioliona hili kulisimamia na kumfikisha mmiliki/dereva sehemu husika ili sheria ifatwe. hilo dataja linawasaidia wananchi wa huko na si tanroad kama unavyofikiri, serikali ni mimi na wewe, tanzania ni jina tu.

    ReplyDelete
  4. Dereva atozwe zinga la fine au anyanganywe kabisa leseni, aah! kumbe nimesahau leseni anaweza pata mpya ndani ya wiki moja kupitia mlango wa nyuma, na fine inaweza kuwa 25,000 tu!!!

    Bila kuchukua hatua kali uzembe na uharibifu barabarani vikiambatana na ajali havita kwisha.

    ReplyDelete
  5. watumiaji wa daraja hilo mlitakiwa mumdhibiti huyo dereva, na siyo kuuliza Tanroads wako wapi.

    ReplyDelete
  6. Yaani huyu dereva ni tahira,natamani daraja livunjike na lori lake kuzama majini kutambua ujinga alioufanya

    ReplyDelete
  7. Tanirod wafanye nini wakati hao jamaa wakipigwa faini wanagoma na kufunga mabarabara? Ngoja liharibike ndio akili itakuja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...