Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akimkabidhi vifaa vya Michezo mmoja wa wanafunzi waliowakilisha shule zao katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom Salum Mwalimu.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Salum Mwalimu(kushoto) akimkabidhi hundi ya mfano yenye thamani ya shilingi Milioni moja Katibu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT) Henry Lihaya leo jijini Dar es Salaam, katikati yao ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel. Msaada huo ni kwa ajili ya kugharamia mahitaji madogomadogo wakati wa mshindano yanayotarajiwa kuanza mapema hivi karibuni.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akizungumza na wadau wa michezo (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa shule 12 za Sekondari kutoka manispaa zote za jijini la Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano yanayotaraji kufanyika mapema hivi karibuni, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom Salum Mwalimu.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Vodacom Salum Mwalimu akizungumza na wadau wa michezo (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa shule 12 za Sekondari kutoka manispaa zote za jijini la Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano katikati ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangarawa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel. Vodacom ndiyo waliodhamini upatikanaji wa Vifaa hivyo.
Baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule zilizokabidhiwa vifaa vya michezo wakifuatilia zoezi la makabidhiano hayo leo jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Frank Shija - Wizara ya Habari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...