Pichani ni magari ya kuzolea taka ngumu ya kampuni mbalimbali yakiwa kwenye foleni ya kuingia Dampo la Pugu Kinyamwezi ambalo miundo mbinu yake ni mibovu na kupelekea zoezi hilo kuchukua zaidi ya siku 4 mpaka kufanikisha kufikia eneo maalum la kumwagia taka ngumu.
.Ni kutokana na kukwama kwa magari ya taka kwenye Dampo la Pugu
.Siku ya tatu sasa magari ya taka yamekwama
Na. Mwandishi wetu,
MIUNDOMBINU mibovu katika Dampo kuu la jiji la Dar es Salaam Pugu Kinyamwezi imesababisha magari makubwa ya kuzoa na kumwaga taka kukwama kwa muda wa siku tatu na kupunguza ufanisi wa kuzoa taka katika mkoa wa Dar es Salaam.
Mtoa taarifa wetu ambaye hakutaka kutajwa kwenye blogu hii, amesema kwamba uongozi wa Dampo Pugu umeshidwa kuweka utaratibu mzuri na kukarabati miundombinu ya dampo kwa muda mrefu na kusababisha msongamano mkubwa wakati wa kwenda kumwaga taka katika sehemu hiyo.
TUNASUBIRI MZUNGU AJE ATUSAIDIE
ReplyDeleteUzuri wanasoma Michuzi; hivyo wameona (wazungu) watakuja kutoa msaada!
ReplyDelete