Mimi na mwanangu Kilian Kamota tunawatakia heri ya mwaka mpya 2014 uwe wa Baraka, furaha, mafaniko, mshikamano na amani kwetu wote.
Salamu hizi zimechelewa kidogo nilisafiri na mume wangu South Africa krismas na mwaka mpya tulikuwa jimboni kwake Limpopo, hayo ndio majukumu ya ndoa.
Tumshukuru Mungu mwaka umepita salama ila tuliwapoteza Tata Mandela na mwanamuziki maarufu wa siku nyingi Tabu Ley ambaye wazazi wangu walipiga sana nyimbo zake nikiwa mdogo sana miaka ya sitini kule Masasi kwa babu yangu Mhindi marehemu mzeee Omari Bellim kulikuwa na santuri zikipigwa sikujua ni nani ila wimbo huo ni ule wa selikutu, na kwa wazazi wangu Dar nako wakipiga sana wimbo huo hadi ukabaki kichwani miaka na miaka.
Tata Mandela huko South Africa wanalia sana, ingewezekana akatarudi ingekuwa furaha kubwa sana nakumbuka wimbo wa Brenda Fassie ngizobuya yaani atarudi, Tata Mandela ni baba na babu wa dunia.
Basi niwatakie tena furaha na amani nyumbani Tanzania! home is sweet! always sweet!
Christina Innocent
Mama Bishanga
Ohio
USA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...