Makamu Mwenyekiti wa CCM,Phillip Mangula akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Mary Mwanjelwa baada ya kuwasili leo asubuhi kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya , tayari akwa maadhimisho ya miaka 37 ya CCM yatakayofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya Jumapili Februari 2. Kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
Mangula (katikati) akiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati) akizungumza na Nape (kulia) pamoja na Zambi kwenye chumba cha watu mashuhuri (VIP) alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Mbeya leo mchana, tayari kwa maadhimisho hayo.
Nape (kulia) akizungumza na Kinana pamoja na Zambi kwenye Uwanja wa Ndege wa Songwe
Dk. Mary Mwanjelwa (kushoto) akijadiliana jambo na Makmu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Dogo Idd Mabrouk wakati wa mapokezi hayo.
Mh. Nape punguza uzito kaka, unakoelekea si kuzuri kwa afya yako.
ReplyDeleteNi ushauri tu.
Sawa, Waheshimiwa Kinana, Zambi na Nnauye mmnasemaje kuhusu Kichwa cha Habari ktk uso wa Gazeti la leo la MWANANCHI analosoma Mhe. Nape Nnauye?
ReplyDeleteHuu ndio wakati wa kumfunga paka Kengele!
Nani atamkata Mkia Simba?
Ujenzi wa Chama cha Mapinduzi kazi tunayo!
Kazi ipo Mbeya, kwa kuwa Magwandazzz yameshamiri sana nafikiri Wanyampala ndugu zetu wamechukulia lile baridi la kule kwao na Msaada wa Chama wa MAKOTI YA KAKHI kama ndio njia ya kulikabili baridi!!!
ReplyDeleteNadhani Wandugu zetu Mbeya meshuhudia ubovu wa Kyadema na fukuza fukuza kiholela za wanachama!
ReplyDeleteHuu ndio wakati wa kuvua Magwandazzz!!!