Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Balozi Rajabu Gamaha (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Asia, Afrika na Oceania kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Colombia, Bibi Sandra Salamanca. katika kikao hicho, viongozi hao walijadili namna Tanzania na Colombia zitakavyoweza kushirikiana ili kutumia fursa zinazopatikana katika nchi hizo kwa madhumuni ya kuinua kipato cha wananchi wao.
Bibi Salamanca (kulia) akisisitiza jambo huku Balozi wa Colombia nchini Tanzania mwenye makao yake Nairobi, Kenya Mhe. Maria Lugenia Correa akisikiliza kwa makini.
Mkurugenzi wa Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu akifafanua jambo katika kikao hicho huku Bw. Graison Ishengoma, Afisa Mambo ya Nje akinukuu masuala muhimu ya mazungumzo. 
Picha ya pamoja, wa tatu kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu ambapo kulia kwake ni Mratibu wa Masuala ya Afrika, Mashariki ya Kati na Asia ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Colombia, Balozi Betty Escorcia.
Picha na Reginald Philip Kisaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Colombia,

    Tanzania ina fursa lukuki za kiuwekezaji na uchumi wa njia za kawaida za kihalali na sio uchumi wa sembe.

    -Njooni tuchimbe madini,
    -Njooni tuendeshe kilimo cha mazao ya chakula na biashara na sio kilimo cha 'unga'
    -Njooni tuendeshe uvuvi,
    -Njooni tutafute Gesi nyingine zaidi na Mafuta,

    -.....

    Karibuni tufanye biashara za kiukweli kweli na sio 'mamizigo mamizigo' maana Colombia INAJULIKANA KUWA ni SHAMBA KUBWA LA KUSINI LA UNGA !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...