Kikosi kazi cha Golden Bush 
Kikosi kazi cha Wahenga FC

Napenda kutoa taarifa kwamba ule mpambano wa marudiano kati ya Golden Bush na Wahenga utapigwa katika uwanja wa TP pale Tandale siku ya kesho kuanzia saa kumi na nusu juu ya alarma. mechi hii ni ya maduriano baada ya ile ya kwanza kushuhudia Golden Bush wakilambishwa mchanga na kukubali kipigo cha goli 1-0. 

Kwa katambua umuhimu wa game hii ya watani wa jadi, tumelazimika kumtafuta refa aliyeobobea katika shughuli za uamuzi wa mpira Tanzania bwana Othmani Kazi ambaye atakuwa mwamuzi wa katikati akisaidiwa na waamuzi wasaidizi watatu. tumelazimika kuwa na waamuzi wa kutosha kama sharia za FIFA zinavyotaka.


Kwa maandalizi tuliyofanya Golden Bush, na kwa kutambua uwezo wa wapinzani wetu, nathubutu kusema kwamba game yako ya kesho huenda tutavunja record tuliyoweka mwaka jana ya kuwafunga goli 4. target yetu ni kufunga goli 3 kila kipindi. tunaweka Malengo hayo kwasababu kesho timu yetu itakuwa sawasawa, wachezaji wetu wote wapo na wako tayari kupiga soka la kufa mtu.

Ni mechi itakayosheheni ufundi, utaalam na mambo ya jadi kwa mbali kidogo ili kuhanikiza ile football ya kiafrika.

Karibuni sana mashabiki ili mje mpate burudani iliyotoka darasani.

Asanteni kwa Kunisikiliza.

Onesmo Waziri "Msemaji wa Golden Bush Veterans"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...