Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni ya abiria iliyopangwa kuondoka leo Alhamisi   Januari 09, 2014 saa 3 usiku kwenda bara  imeahirishwa  hadi kesho siku ya  Ijumaa   Januari 10, 2014, saa 10 jioni.
Taarifa imefafanua kuwa dharura hiyo imetokana na eneo la reli kati ya  stesheni za Godegode na Gulwe  mkoani Dodoma kukumbwa na mafuriko usiku wa kuamkia leo.

Wahandisi na Mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio tokea jana  usiku na taarifa za uhakika zinaeleza kuwa  zoezi la kukarabati litakamilika saa 10 leo jioni ( Alhamis Januari 09, 2014).

Aidha taarifa  hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza..

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Paschal Mafikiri.
TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Januari 09, 2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. SIJUI LINI UMASIKINI HUU UTAKWISHA, MANAKE TUKO ENZI ZA UJIMA BADO

    ReplyDelete
  2. Basi watume za mizigo jamaniiiii ah

    ReplyDelete
  3. na nyie kampuni ya reli wakati umefika, mbadilike sasa. abiria wakija kukata tiketi chukueni na namba zao za simu ili kama kuna mabadiliko muwajulishe, mtu anatoka mbali kuja rly stesheni anakuta imeahirishwa kwa siku hiyo, na vichapati vyake na watoto, ni usumbufu kweli!!! kuna kabang, airtel yatosha, cheka time ...., jiungeni mtume messages kwa abiria wenu. bado mko zama za kale tu! ndo maana hata wafanyakazi wenu wachovu sana hawana hata maendeleo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...