Wananchi mbalimbali wakipata maelezo ya kina juu ya umuhimu wa
taarifa za hali ya hewa katika banda la TMA kwenye maonesho ya maadhimisho
ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Meneja Kituo cha Zanzibar Bw. Said Khamis akimwelezea mwananchi
njia mbalimbali za ukusanyaji wa takwimu za hali ya hewa kwenye maonesho ya
maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ofisa Uhusiano wa TMA Bi.Monica Mutoni akitoa elimu kwa umma
jinsi ya kupata taarifa za hali ya hewa kupitia njia mbalimbali za usambazaji wa
taarifa hizo kwenye maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Mkurugenzi wa ofisi ya Zanzibar, Bw Mohamed Ngwali akitoa
maelezo ya takwimu za hali mbaya ya hewa iliyowahi kutokea kwa kipindi cha
miaka 50 katika visiwa vya Unguja na Pemba, akisisitiza wananchi kutopuuza
tahadhari zitolewazo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...