Na Athumani Shariff

Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe leo amekutana na balozi wa Ubelgiji Koen Adam makao makuu ya Wizara ya Maji, Ubungo jijini Dar es Salaam kujadili mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya maji.

Profesa Maghembe alimuomba Balozi Adam asaidie wilaya ambazo zinakabiliwa na matatizo makubwa ya uhaba wa maji, ambazo aliziainisha kuwa ni Makambako, Songea, Wanging’ombe na Makonde ambapo jumla ya Dola 20,000,000 za Marekani zinahitajika kutatua shida hizo.

Wakati wa mazungumzo hayo, Profesa Maghembe alisema wananchi haswa waishio vijijini wanapata tabu sana kutokana na shida ya maji. “Wananchi wanapata tabu sana kupata maji, inawagharimu kati ya saa moja hadi mbili kuchota ndoo moja ya lita ishirini, hivyo ili kukamilisha mahitaji ya matumizi ni wazi kuwa muda mwingi utatumika na hatimaye kuzorotesha shughuli nyingine za uzalishaji”. Alisema Waziri Maghembe.

Akijibu swali la Balozi Adam juu ya maswala ya umeme, Profesa Maghemebe alisema hiyo ni changamoto kubwa sana kote mijini na vijijini. Gharama za Tanesco na zile za Diseli zipo juu. Alisema tayari amemuagiza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mbogo Futakamaba na baadhi ya wataalamu kutoka wizarani kwenda nchi za Uchina na Jamhuri ya Watu wa Czech kutafuta kampuni zinazojishughulisha na umeme wa nguvu ya jua (Solar Power) ili miradi yote ya maji vijijini itumie umeme wa jua ili kuwapunguzia gharama za maji wananchi na hiyo kuifanya kuwa ndiyo sheria.

Waziri pia alieleza umuhimu wa upatikanaji wa maji safi katika kukabiliana na afya bora kwa wananchi. Alisema, baada ya kuanza kutumika mradi mkubwa wa maji wa Kahama Shinyanga sasa zaidi ya asilimia 80 ya watu hawendi hospitali juu ya magonjwa mbalimbali yaliyokuwa yanawasumbua awali. Hivyo maji yanamchango mkubwa katika kuboresha afya za wananchi alisisita Profesa Maghembe.

Pia alisema kwa kuwapatia wananchi huduma ya maji safi karibu na makazi yao ni njia kubwa kutika kuwainua kiuchumi, kwani muda mwingi ambao wangeutumia katika kutafuta maji watafanya shughuli nyingine za kiuchumi, hivyo kupandisha kipato chao.

Akielezea maswala ya utunzaji wa vyanzo vya maji, Profesa Maghemebe alisema ni moja ya changamoto tunazokabiliananazo, maji hupungua ingawa mahitaji yawatu huongezeka hivyo jitihada zetu kubwa sasa kwakupitia Idara ya Rasilimali za maji ni kutunza vyanzo vya maji ili haya yaliopo sasa yaendeleee kuwepo kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Waziri wa Maji.
    Dar es salaam kwenyewe hakuna maji,
    Lol, Bongo bwana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...