Je, rasimu ya Katiba mpya imeongeza nini na imepunguza nini katika kumkomboa mwanamke? Msikilize hapa Profesa Ruth Meena akizungumzia jinsi mwanamke alivyopewa kipaumbele katika rasimu hii na ameelezea kundi gani limezungumziwa na kuongezwa kwenye rasimu hii ambayo imesahau makundi kama watoto wa kike, wazee na kusahau wanaathirika vipi katika jamii yetu ya Tanzania. Pia, amegusia kuwa nchi hii ina rasilimali nyingi zinazoweza kumlinda mwanamke na vizazi vyake. 

 Tazama video hapa chini:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Dada Joyce nakupongeza kwa kuturishia hiki kipindi kizuri na muhimu sana katika wakati huu ambapo taifa letu linaweka historia. Nampongeza mama yetu prof. Ruth kwa kuwaelimisha wanawake. Tanzania tumekuwa wa mwisho katika kila kitu tukifananishwa na nchi zingine za Afrika mashariki. Tuko nyuma kwenye mambo ya haki za akina mama na watoto, urai pacha n.k. sijui hili ni kwanini? Muda umefika wa sisi kujiuliza ni kwa nini? Napenda kuwajulisha akina mama kwamba wanauwezo mkubwa sana wa kuweza kumchagua kiongozi kwa mfano mbunge anayejali haki za akina mama na watoto. ukiangalia sensa za taifa, Tanzania ina wanawake wengi kuliko wanaume. Sasa kama mgombea hatakiri wakati wa kampeni zake kwamba yeye atapigani haki zenu kama wanavyofanya huko USA na nchi zingine kwanini mnampa kura zenu? wanaharakati wa haki za mama na watoto waelimisheni wanawake waelewe kwamba wana nguvu kubwa sana ila hawajaitumia. Bwana Kapuya amebaka yuko nje mpaka leo serikali haijatamka chochote kuhusu hilo swala, wanaharakati mmefanya nini? Huo mfano unatakiwa ufikiswe kwenye bunge la katiba ili pawekwe sharia dhidi ya viongozi wanaotumia madaraka yao kuvunja haki za binadamu haswa wanawake.

    Mdau

    Kaka M

    ReplyDelete
  2. The mdudu,sasa mnalalamika nn? Wakati tayari rais ashafanya kila kitu kipo 50,50 wanawake na wanaume wako sawa hapa ni kujipanga tu kilicho baki na sivinginevyo,ila hao akina mama walioteuliwa kama watajibweteka na hizo poshoozzzz basi hakuna kitakacho badilika coz kama haki za msingi za akina mama,watoto,wazee hazitawekwa au kuzizungumzia huko bungeni basi wao watoke bungeni kwa kila kikao hiyo ndio itakua dawa ya hayo matatizo,ila wakisema sitoki coz ntapoteza poshooozzzz zangu basi wakae wakijua ya kwamba watawaponza wanawake woote waendelee kuteseka kwenye nchi yao yenye neema tele,huyu mama profesa anaongea mambo ya umuhimu sn kwenye kuwatetea wanawake wote mamaangu nakupenda sn na mungu akulinde akupe afya tele kabisa,

    ReplyDelete
  3. Apewae ndie aongezwae.Kwani kinamama Tanzania si mnazo nafasi za upendeleo nyie bungeni wakati kina baba hawajapewa. Katika haki sawa kwa wote na nyie bora mpiganie kama wanaume.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...