Na Abdulaziz Video, Mtwara
Kongamano kubwa la Viongozi wa Dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara lililoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini limeanza leo katika manispaa ya Mtwara/mikindani kwa Viongozi hao pamoja na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kwa kutembelea eneo la Mnazibay/Msimbati sehemu ambayo imegundulika gesi asilia pamoja kukagua ujenzi wa eneo la uchakataji wa Gesi hiyo.
Katika ukaguzi huo Viongozi hao wakiongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Bw Eliakim Maswi baada ya kuzungukia miradi mbalimbali ya Gesi na Mafuta kesho kutafanyika kongamano litakaloshirikisha Viongozi hao wa Dini na Viongozi wa serikali akiwemo mkuu wa mkoa wa Lindi na Mtwara Kauli mbiu ya kongamano hilo ni RASILIMALI ZETU ZA GESI ASILIA,MAFUTA NA MADINI KWA AMANI NA MAENDELEO YA TAIFA.
Kongamano hilo linashirikisha zaidi ya wadau 200 kutoka mikoa hiyo ya lindi na Mtwara wakiwemo maofisa wa wizara na serikali za mikoa hiyo pamoja na wanahabari.
Katibu mkuu wa wizara ya Nishati na Madini,Eliakim Maswi (wa pili kushoto) akiongozana na Viongozi wa Dini walipokuwa wakikagua mradi wa Gesi katika eneo la Msimbati.
Baadhi ya viongozi mbali mbali wa dini wakitembelea eneo la Mnazibay/Msimbati sehemu ambayo imegundulika gesi asilia pamoja kukagua ujenzi wa eneo la uchakataji wa Gesi hiyo.
Mitambo iliyopo kwenye eneo hilo.
Ujenzi ukiendelea.
Waandishi wa habari wakiwa katika basi kuelekea eneo la msimbati na Madimba kwa ajili ya kujionea mitambo ya gesi na ujenzi unaoendelea katika vijiji vya msimbati na Madimba
Baadhi ya wanahabari wakiteta na Katibu mkuu wa nishati na madini mara baada ya kuwasili katika eneo la Madimba kukagua ujenzi wa sehemu ya kuchakata gesi na majumba ya wafanya kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...