Na Mwenekaya Said,Globu ya Jamii - Kisutu
KESI ya mauaji ya kukusudia inayomkabili Mfanyabiashara maarufu nchini,Marijan Abubakar maarufu kama Papa Msofe (50) na mwenzake Makongoro Joseph Nyerere katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, bado inafanyiwa kazi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kwa ajili ya hatua zaidi.
Kesi hiyo imeahirishwa leo, na Hakimu Mkazi Hallen Riwa amesema kwa kuwa jalada la kesi liko kwa DPP na kwamba washtakiwa wanatakiwa kuwa na subira.
Hakimu Riwa alisema kesi hiyo ilitajwa Februari 25, mwaka huu kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
Kabla ya kupanga tarehe hiyo, mshtakiwa wa pili Makongoro aliulalamikia upande wa Jamhuri kuwa unachelewesha upelelezi wa kesi yao kwa makusudi na kwamba wao wamekaa muda mrefu gerezani wanateseka.
Msofe ambaye kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani hapo Agosti 10, mwaka 2012 anadaiwa kuwa yeye pamoja na mwenzake Makongoro, Novemba 6, mwaka 2011 huko Magomeni Mapipa kwa kukusudia walimuua Onesphory Kitoli.
Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao walifanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka ya mwaka 2002.
Jela kumempenda jamaa; naona ametoka mchicha haswa.
ReplyDelete