Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na
Kozi fupi, 
Bwana, Juma M. Kanuwa
  
CHUO CHA DIPLOMASIA DAR ES SALAAM, katika kuendeleza wito na wajibu wa kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu, mnamo tarehe 31st March - 4th Aprili 2014 kitafanya kozi fupi ya ITIFAKI NA MAHUSIANO YA UMMA (PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS) Chuoni Kurasini, Dar es salaam,
Wawezeshaji wa Mafunzo haya ya muda mfupi kawaida huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea sana katika mambo ya Diplomasia hivyo kuwapa washiriki uzoefu na kesi halisi zilizowahi kutokea katika eneo husika la mafunzo ili kuwajengea uwezo na waweze kwenda kufanyia kazi moja kwa moja mafunzo na utaalam walioupata.

Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi, Bwana, Juma M. Kanuwa akilisisitiza kwamba kutokana na umuhimu wa utaalam wa mambo ya ITIFAKI NA MAHUSIANO YA UMMA (PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS) katika sehemu za kazi, mafunzo hayo yatarudiwa tena tarehe 31st March - 4th Aprili 2014, alisema;
 “CHUO CHA DIPLOMASIA kilifanya mafunzo haya mnamo tarehe 3rd – 7 Februali 2014, lakini kutokana na maombi ya wengi na kwakuwa mafunzo haya ya PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS ni muhimu sana hasa eneo la ‘PROTOCOL’,  yatarudiwa tena mnamo tarehe 31st March - 4th Aprili 2014 hapa hapa Chuo cha Diplomasia ili wale wote walioshindwa kuhudhulia hapo awali waweze kuja kwa wingi chuoni na kupata mafunzo hayo toka kwa mabalozi na wataalam waliobobea na wenye uzoefu wa miaka mingi…” 
Akaongeza kuwa  “..nafasi zimebaki chache hivyo nawashauri wale wote wanaotaka kushiriki mafunzo haya waje Chuo cha Diplomasia au wawasiliane na mratibu kwa namba +255713667303 na pia watembelee tovuti ya chuo cha Diplomasia www.cfr.ac.tz kwa maelezo na tangazo la kozi hii…”                                                                                                 
Mafunzo haya ni muedelezo wa mafunzo ya muda mfupi yaani ‘kozi fupi’ zinazofanywa na CHUO CHA DIPLOMASIA – DAR ES SALAAM, kila mwezi ambapo kozi mbali mbali zimekuwa zikifanyika, kama Utatuzi wa Migogoro “CONFLICT RESOLUTION AND MEDIATION” na Usalama wa taarifa ( INFORMATION SECURITY) iliyofanyika mapema hivi karibuni.
Pia CHUO CHA DIPLOMASIA kinaweza kufanya kozi kulingana na mahitaji ya taasisi/ wateja na kinakaribisha wadau wote
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi,
Mobile: +255713229722, +255713667303                                  
Website:  www.cfr.ac.tz    
E-mail:  lucassoona@yahoo.com


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Habari na pole na majukumu ndugu yangu. Awali ya yote naomba kujua utaratibu wa kusoma katika chuo cha diplomasia kwa mtu mwenye ufaulu wa division four. Asante

    ReplyDelete
  2. Habari zenu naomba kujuwa juzi kozi za muda mfupi zinazotolewa chuo cha kidiplomasia na vile vile zinachukuwa gani naomba majibu

    ReplyDelete
  3. Habar zenu naomb kujua jinsi ya kujiung na chuo ngaz ya certificate

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...