.jpg)
----------------------------------------
Na Frank Mvungi-MAELEZO
Tanzania ni
miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa
magadi soda yatakayoingizia taifa Shilingi Bilioni 480 kwa mwaka, imefahamika.
Meneja Uhusiano na Mawsiliano wa Shirika la
Taifa la Maendeleo (NDC), Bw. Abel Ngapemba alisema leo kuwa hatua hiyo inatokana na kugunduliwa kwa kwa kiasi kikubwa cha madini
hayo katika Bonde la Engaruka Wilayani
Monduli mkoani Arusha.
Alizitaja
faida za kugundulika kwa madini ya magadi soda kuwa ni ajira zaidi ya 500 na
fedha za kigeni kutokana na mauzo ya
madini hayo nje ya nchi.
Alisema
kuwa viwanda vinavyotegemea magadi soda kama malighafi ya uzalishaji hali
itakayochochea kukua kwa sekta ya viwanda hapa nchini.
Bw. Ngapemba alibainisha kuwa madini ya magadi soda
yanatumika viwandani katika utengenezaji
wa bidhaa kama vioo, sabuni, dawa za meno, dawa za hosipitali, uoakaji mikate, kutengeneza karatasi, nguo, na usafishaji wa maji.
Alifafanua
kuwa utafiti uliofanywa na wataalamu wazalendo kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 na
ulifanyika kwa awamu tatu yakwanza ikiwa
ni uchunguzi wa awali na kutafuta maeneo ya kufanyia uchorongaji ili kubaini
wingi na ubora wa magadi soda.
Alisema
kuwa kazi ilifanywa na kampuni ya OC, na kwamba awamu iliyofuata ni kuangalia
njia ya uvunaji wa magadi soda hayo iliyofanywa na JSC Service.
“Matokeo
ya utafiti huo yameonyesha kuwapo kwa magadi soda kiasi cha mita za ujazo
bilioni 4.7 na inakadiriwa kila mwaka wastani wa mita za ujazo milioni 1.9 zinaongezeka
katika eneo hilo”, alisema Ngapemba.
Alisema
kuwa NDC itahakikisha kuwa katika utekelezaji wa miradi hii mazingira
hayataathiriwa na tunu za taifa zitalindwa ambapo mtazamo wa shirika hilo ni
kuwapo kwa mradi wa uvunaji magadi, utalii, na ufugaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...