Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kutoa agizo kwa viongozi na watendaji wa jiji la Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanawaondoa na kuwachukulia hatua za kisheria wanaovunja sheria za jiji kwa kuendesha shughuli mbalimbali katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna (CP) Suleiman Kova akitoa ufafanuzi ameeleza kwa waandishi wa habari kuhusu wakazi wa jiji la Dar es salaam hususan madereva wa bodaboda na Bajaji kufuata sheria za barabarani na kajenga tabia ya kufanya tathmini ya safari zao iwapo wanakidhi vigezo vya usalama barabarani ili kuepusha madhara.
Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Mashariki Bw. Conrad Shio akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu sheria inayosimamia usafiri wa Bajaji na Bodaboda nchini. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Yetu macho, tukisubiri utekelezaji wa haya maagizo na kuona utekelezaji utadumu kwa muda gani.

    ReplyDelete
  2. Hivi hawa waheshimiwa wanakatanza bodaboda na bajaji na hawana solution mdadala ya kujikwamua na tatizo la foleni wanaakili timamu kweli. ndio tunajua bodaboda na bajaji ni kero katikati ya mji lakini sisi wananchi tusiopita na ving'ora zinatusaidia, wawe wanakuja na solution kwanza ndio waondoe bodaboda mf kujenga barabara za kutosha ili tuje na kuondoka na magari yetu. waache kuwa useless namna hii.

    ReplyDelete
  3. Viongozi wetu hebu mtufikirie na sisi wa hali ya chini japo kiduchu uwezo wa kipato changu ni kumiliki bodaboda inasaidie kuwahi kazini kutokea mabwepande leo unanikataza nisiingie nayo mjini???? Naomba hili liangalie upya ikibidi basi na muda wa kuripoti kazini usogezwe mbele mpaka saa tatu na nusu asubuhi.

    ReplyDelete
  4. Think first Financially and Economically!!!:

    Boda boda ni Kazi inayotambulika kihalali kutoka na kuwa Wizara ya Fedha ambayo ndiyo muhimili wa kila kitu imeondoa Kodi kwao.

    Hivyo kama Wizara nyeti kama hiyo kwa kitendo hicho ina maana Shughuli za Bodaboda zina akisi Ufanisi wa maisha ya Kiuchumi na Kifedha ktk nchi hivyo ni Huduma muhimu wanayotoa Jijini.

    Isitumike Siasa bali itumike Sayansi kwa maamuzi haya, kama msimamo ni huo (KUWAPIGA MARUFUKU KUINGIA KATIKATI YA JIJI) utolewe Mbadala mwingine wa watoa huduma (AMA TARATIBU MBADALA) wa kuchukua nafasi Bodaboda kabla usitishaji wa huduma zao haujaathiri ufanisi wa kifedha na kiuchumi kwa watu na Biashara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...