Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ameingilia kati Mgogoro wa ardhi uliokuwa ukifukuta kwa muda mrefu katika kijiji cha Mawenzusi,wilaya ya Sumbawanga mjini.Mgogoro huo uliohusu Wananchi na anayedaiwa kuwa Mwekezaji inaelezwa kuwa maamuzi yalikwishatolewa na Mh.Rais Jakaya Kikwete,kuwa Wananchi wapewe kipao mbele na Mwekezaji apewe kiasi,lakini mpaka sasa hakuna lililotekelezwa kufuatia Watendaji waliokuwa wamepewa dhamana ya kulisimamia jambo hilo kusua sua na hatimaye kutopatiwa ufumbuzi wa haraka.

Kinana yuko mkoani humo kwa ziara ya siku sita ya kuangalia uhai chama,miradi na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa hongera sana. Mbona hujatamka kuwa aliyehusika achukuliwe hatua? Hotuba hiyo siku moja uitoe kwa baraza lenu la mawaziri...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...