Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Alex Msama akizungumza na baadhi ya Wanahabari kwenye moja ya mikutano yake kuhusiana na tamasha la pasaka.
KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, mwishoni mwa wiki ilitangaza viingilio vya tamasha hilo jijini Dar es Salaam, viti vya kawaida ni shilingi 5000 na watoto 2000. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Alex Msama viti maalum ni shilingi 20,000 wakati VIP  ni shilingi 10,000.
 Msama alisema hivi sasa wanaendelea na mchakato wa kufanikisha zoezi la mgeni rasmi katika tamasha hilo kwani hivi karibuni watakamilisha zoezi la upigaji kura kumchagua.
Msama alisema mchakato wa kuelekea katika tamasha hilo litakalofanyika jijini Dar es Salaam Aprili 20 na baadaye mikoa mingine saba hapa nchini.
 Aidha Msama alitoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kujiandaa na tamasha hilo ipasavyo kwani lina mlengo wa kurudisha mapato yanayopatikana na kuyapeleka katika maeneo matatu ambayo yanawahusu, yatima, walemavu na wajane.

 Msama alisema mipangilio yake ya kuwawezesha wenye uhitaji maalum ni kuwajengea kituo kitakachokuwa katika eneo la Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambacho kitajulikana kama Jakaya Mrisho Kikwete, rafiki wa wasiojiweza.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...