Huku ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiwa inaelekea ukingoni mdhamini Mkuu wa ligi hiyo  Vodacom Tanzania, wamesema wanavutiwa na ushindani ulipo katika mechi za sasa za ligi na mbio za ubingwa.

Akizungumza punde baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Yanga na JKT Ruvu iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na Yanga kuibuka na Ushindi wa Mabao 5 – 1. Meneja Uhususiano wa Nje wa Kampuni hiyo, Salum Mwalimu amesema kuwa, mafanikio waliyo yatarajia kutokana na udhamini wa ligi kuu yameanza kuonekana na kufurahia kuwa sehemu ya mapinduzi ya soka nchini.

“Ukiangalia namna ushindani ulivyo sasa ni dhahiri kuwa ligi yetu imefikia patamu na haya ndio mafanikio tuliyokuwa tunayataka, kila timu inajitahidi kwa hali na mali kuhakikisha inashinda mechi zilizobaki ili kuchukua Ubingwa au kutoshuka daraja:, alisema Mwalim

“Tukianza na mbio za ubingwa sasa ni wa aina ya kipekee kati ya Azam, Yanga na Mbeya City, tunashuhudia namna timu zote zinavyo hangaika kuhakikisha zinanyakua pointi zote tatu ili kujiweka mahala azuri pa kuchukua Ubingwa, tumebakiza mechi tatu lakini hadi sasa bado hatujajua bingwa ni nani, sio kama ilivyokuwa zamani,” alisema Mwalim na Kuongeza.

“Hili ndilo tulilokuwa tunalitarajia tangu zamani, kuona timu zidi zinakuwa katika nafasi ya kuwania ubingwa na hata kutokuwa na uhakika wa kushinda katika mechi zote walizobakiwa nazo, Iwe Yanga, Azam au, Simba wote wakienda Mbeya, Kagera, Morogoro Tanga au Arusha hawana uhakika wa kutoka na ushindi ni jambo la kuvutia sana” alisema Mwalim.

Meneja huyo alihitimisha kwa kuzitkia nafanikio timu zote za ligi kuu kuwa na mafanikio katika mechi zilizobaki huku akitanabaisha kuwa zawadi za msimu huu zitatolewa mapema na zimeboreshwa zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...