Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tuzo iliyopata hivi karibuni ya ubora wa kimataifa Dar es Salaam.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionyesha moja ya tuzo za dhahabu ilizowahi kupata wakati wa mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tuzo iliyopata hivi karibuni ya ubora wa kimataifa Dar es Salaam.

Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza ushindi wake wa tuzo la Ubora wa Kimataifa 2014 maarufu kama ‘International High Quality Trophy 2014’ katika mashindano ya Monde Selection. Safari Lager itapokea tuzo hiyo Jumatatu tarehe 2 Juni, mjini Bordeaux, Ufaransa.

Tuzo ya Ubora wa Kimataifa au ‘International High Quality Trophy’ ni tuzo ya heshima linalotolewa kwa bidhaa ambazo zinashinda tuzo za ‘Gold’ au ‘Grand Gold’ kwa zaidi ya miaka 3 mfululizo. Safari Lager inepewa tuzo hiyo ya heshima kwa kuweza kushinda ‘Gold’ na ‘Grand Gold’kwa zaidi ya miaka mitatu mfululizo.

Akizungumuza na waandishi wa Habari, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Bw. Oscar Shelukindo, alisema, “Safari Lager ni bia ambayo siku zote nia yake ni kuridhisha wateja wake na kwa miaka yake yote…Tunaishukuru sana Monde Selection kwa heshima waliyotupa na hii inatupa motisha ya kuendelea kuwapa wateja wetu bia bora zaidi”.

Bw. Fimbo Butullah, Maneja Masoko wa Safari Lager aliongezea kwa kusema, “Tungependa tena kuishukuru Monde Selection kwa heshima waliyotupa, wateja wetu na kwa Watanzania kwa ujumla. Sisi Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager kwa kufika hapa tulipo sifa hizi si za TBL peke yake ni za Watanzania kwa ujumla na haswa wateja wtu wanaotumia bia ya Safari Lager”.

Fimbo alimaliza kwa kutoa wito kwa wateja wa Safari Lager kuendelea kutumia bia hiyo kwani ndio bia namba moja kwa ubora na kwa mauzo Tanzania na pia ni bia namba moja Afrika na leo hii tunapozungumza imepata heshima ya pekee ya ubora wa kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...