WATU 17 wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu Mkazi jijini Arusha, kujibu mashitaka 16 yakiwemo ya kuua kwa kutumia bomu,kutesa
binadamu na kusajili vijana na kuwapeleka nje ya nchi kufanya ugaidi.
Watu hao walifikishwa mahakamani hapo leo na kusomemewa shitaka hilo
mbele ya Hakimu Mkazi Mustafa Siama ambapo hawakutakiwa kujibu chochote
kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa
kusikiliza kesi hiyo.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda tukio hilo Aprili 13,katika nyumba ya
kulala wageni na baa ya Arusha Night Park iliyopo Mianzini jijini
hapa,ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi juni 11 mwaka huu kwa
mtuhumiwa namba moja na namba nne na watuhumiwa wengine waliobaki kesi
yao itatajwa tena
juni 12
Katika tukio hilo la mlipuko huo wa bomu watu 14 walijeruhiwa vibaya
katika maeneo mbalimbali ya miili yao hali iliyopelekea mmoja wa
majeruhi hao aliyefahamika kwa jina la Sudi Ramadhani mkazi wa
Kaloleni jijini hapa kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika
hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.
Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Polisi Arusha,kabla
ya watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani,Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai nchini (DCI) Isaya Mngulu amesema kuwa mara tu baada ya kutokea kwa
tukio hilo, polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama
walianza upelelezi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.
Ameongeza kuwa pia siku hiyo hiyo ya tukio hilo la mlipuko wa bomu
katika baa ya Arusha Night Park muda mfupi baadae bomu lingine la
aina ileile liligundulika kutegwa katika baa ya Washington ya jijini
hapa ambapo bomu hilo liliondolewa katika eneo hilo bila kuleta
madhara .
"Aidha baadhi ya watuhumiwa hawa pia walibainika kuwa na mikakati ya
mashambulizaya namna hiikatika maeneo mengine na sehemu mbalimbali
hapa nchini ambazo ni taasisi za Serikali na sehemu zenye mikusanyiko
ya watu,ambapo pia wanajihusisha na uandaaji wa vijana kutoka mikoa
mbalimbali hapa nchini na kuwapeleka nchi za nje ili kujiunga na
makundi ya kiuhalifu"alisema Mkurugenzi huyo wa Mashitaka nchini.
Mkurugenzi huyo amesema kwamba upelelezi wa matukio haya bado
unaendelea ili kuwakamata watiliwa shaka wenginewaliobaki katika
matukio ya milipuko ya mabomu katika Kanisa Katoliki Olasitna uwanja
wa Soweto yaliyotokea mwaka jana jijini hapa na sehemu nyingine
nchini.
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la
polisi kwa lengo la kuwafichua wahalifu wa ndani na nje wa matukio
haya ya kihalifuna matukio mengine kwa lengo la kuvuruga amani na
utulivu wan chi.
Mmoja wa watuhumiwa hao akipakiwa kwenye Gari la Polisi tayari kwa Kupelekwa Mahakamani kusikiliza kesi yao.
Watuhumiwa wakiwa kwenye gari ya Polisi.
Tatizo kubwa ni njaa !
ReplyDeleteWadhamini wa Ugaidi hutoa fedha ktk DOLLA ZA MAREKANI sio Tanzania Shilingi, ndio maana usipokuwa makini ukiendekeza njaa, na tamaa bila kutazama kwa urefu unaweza kupokea Dola zao hizo zikakufikisha kama hapo!