Jeshi la polisi mkoani Lindi linamtafuta askari wake mmoja mwenye
namba F6508 Detective Constable JOSEPH YONA MASANJA mwenye Umri wa
miaka 34 mzaliwa wa Wilaya ya ILEMELA Mkoani MWANZA Abae alikuwa
akifanya kazi kituo cha polisi KILWA kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa
vipande 62 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 568 yaliyokuwepo
kituoni hapo kama Vielelezo.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi,Kamishna
Msaidizi Renatha Mzinga alipokuwa Akitoa taarifa kwa waandishi wa
habari kufuatia jitihada mbalimbali za kumtafuta kutoleta Mafanikio.
Mtuhumiwa Huyo ambae alikuwa mtunza Vielelezo katika kituo cha polisi
Wilayani Kilwa toka mwaka 2004 ambaye kwa sasa amefukuzwa kazi
kutokana na utoro kazini ,kabla ya kugundulika kwa wizi huo baada ya
kuomba ruhusa ya kwenda kusoma Chuo Kikuu cha DSM ambako baada ya
uchunguzi alibainika kuwa alibadili chuo na kwenda chuo kikuu cha SAUT
-Mwanza ambako hata hivyo amebainika ametoweka.
Kufuatia kutoweka kwake Jeshi la polisi mkoani LINDI limewaomba
wananchi kutoa taarifa za mtuhumiwa huyo popote watakapomuona kwani
ametumia nafasi yake vibaya na kuhujumu rasilimali za taifa kwa
manufaa yake binafsi.
'ndg zangu wanahabari naomba mtusaidie maana Huyu jamaa Mara ya mwisho
alikuwa Chuo cha SAUT cha Mwanza tulipomfuatialia akawa ametoweka
ghafla na suala tulilibaini baada ya vielelezo hivyo kukataliwa
mahakamani na maafisa wanyamapori kuwa si vyenyewe na vina upungufu
mkubwa ikiwemo kupunguzwa ukubwa wake.
Katika tukio lingine Kamanda Mzinga alieleza kuwa polisi wamemkamata
SAID ALLY MASOUD katika kisiwa cha POMBWE wilaya ya KILWA akiwa
amejeruhiwa vibaya na bomu alipokuwa akivua samaki kinyume cha sheria
kwa kutumia baruti.
Mtuhumiwa huyo amelazwa katika hospitali ya KILWA ya KINYONGA na hali
yake imeelezwa kuwa ni mabaya kiasi cha kushindwa kujieleza baada ya
baruti kumfyatukia yeye badala ya samaki.
kuhusu hayo meno isije ikawa kwa kuwa wamesalitiana ndiyo maana anatautwa; wananchi yetu macho tu manake anayekamata mwalifu ni polisi; anayempeleka mhalifu mahakamani polisi; uchunguzi polisi; n.k.
ReplyDelete