Mkuu wa Ushirikiano wa Usalama kwa Ubalozi wa Marekani Tanzania, Lt.Kevin Balisky akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereira Silima wakati wa halfa ya kukabidhi mtambo wa mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa jeshi la maji, masaada huo umetolewa na Serikali ya Marekani kupitia mradi wa AFRICO,leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Pereira Silima, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa ya kukabidhi mtambo wa mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa kikosi cha askari wa maji akitoa shukrani kwa Mkuu wa Ushirikiano wa Usalama kwa Ubalozi wa Marekani Tanzania, Lt.Kevin Balisky wa pili kushoto leo jijini Dar es Salaam, , anayesikiliza ni bw. Norman wa Ubalozi wa Marekani.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani, Pereira Silima (kulia) akizindua mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa kikosi cha askari wa maji katika halfa iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkuu wa Ushirikiano wa Usalama kwa Ubalozi wa Marekani Tanzania, Lt.Kevin Balisky,mtambo huo umetolewa na Serikali ya Marekani kupitia mradi wa AFRICO kwa ajili ya kusaidia kudhibiti uhalifu wa majini na kuweza kutambua vyombo na shughuli zote zitakazofanyika katika maji.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Pereira(kulia) Silima akisiliza maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa mawasiliano Norman(katikati) kuhusu utendaji kazi wa mtambo wa mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa ajili ya kudhibiti usalama wa majini kwa kikosi cha askari maji leo jijini Dar es Salaam, anayeangalia kushoto ni Mkuu wa Ushirikiano wa Usalama kwa Ubalozi wa Marekani Tanzania, Lt.Kevin Balisky.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Pereira Silima, (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja ya viongozi wa jeshi la Polisi na Mkuu wa Ushirikiano wa Usalama kwa Ubalozi wa Marekani Tanzania, Lt.Kevin Balisky (wa tatu kulia waliokaa) katika halfa ya kupokea msaada wa mtambo wa mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa kikosi cha askari wa maji katika halfa iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha Burudani kikitumbuiza katika halfa ya kukabidhi mtambo wa mfumo wa mawasiliano wa masafa marefu kwa ajili ya kudhibiti usalama wa majini kwa kikosi cha askari maji leo jijini Dar es Salaam. Picha na Lorietha Laurence-Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...