Mfano wa mitungi midogo ambayo haikutimia uzito unaotakiwa.
 Salaam Ankal Michuzi.
Tafadhali wahadharishe wadau kuhusu udanganyifu mkubwa unaofanyika hivi sasa kwenye mitungi ya gesi ya kupikia.
Wajanja hao hupunguza gesi kutoka kwenye ile mitungi mikubwa na kupata mitungi midogo ambayo haijatimia uzito unaotakiwa.
Jinsi ya kukwepa udanganyifu huu mkubwa ni  kuwa,  kila unaponunua gesi ya kupikia, kuhakikisha mtungi huo una "seal" kwenye sehemu ya kutolea gesi.
Pili, usinunue mtungi wa gesi bila kuhakikisha kuwa umeupima kwenye mizani iliyopo kwa muuzaji wa gesi. 
Ni matakwa ya sheria kwamba, kila muuzaji wa gesi ya kupikia, anakuwa na mizani dukani kwake ili mteja aweze kuhakiki uzito wa mtungi anaponunua.

Tafadhali mweleze rafiki,  ndugu, jamaa, jirani na hata wenzako kazini au kwenye sehemu ya biashara, ili wasikumbwe na wizi huo wa mchana.
Tafadhali Ankal wajuze wadau wako wajihadhari, kwani taasisi husika (Wakala wa Vipimo) hata wakiwa wengi kiasi gani hawawezi kufika kila kona ya nchi hii ili wafanye kaguzi za kuwabaini Wajanja kama hao.
Ni mimi, Mdau  wa Gesi.


Jinsi gesi inavyopunguzwa toka kwenye mitungi mikubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2014

    Mtanzania kwa Wizi?, ohhh ana akili za kupitiliza !!!

    Jamani Sekta na masuala ya haya siyo ya kwetu sisi ni KURUKA NA UNGO NA CHUMA ULETE, lakini kwa akili za ajabu tumeweza kuifikia Sekta na kufanya Usanii hadi kwenye Gesi !

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2014

    Mhhh, tusione hadi Wasaidizi na Vibarua wa Vituo vya mafuta wanamiliki magari, kumbe mule mule?

    Ama kweli ugumu wa maisha kipimo cha akili!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2014

    Wapelekwe kwa Profesa Muhongo hao halafu awahamishie Mtwara kwenye Gesi!

    Wala msiwakamate na kuwafunga ndio rasilimali zenyewe hizo, tunapata shida kubwa kutafuta Wataalamu wa Gesi nchi za nje kumbe kumbe vipaji adimu tunavyo humu humu nchini wamejaa vituo vya Mafuta!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2014

    Unakuta Mwizi huyohuyo alipokuwa akisoma Shuleni Sekondari, alifeli ktk somo la Physics, hakupenda kusoma kabisa, ama hata masomo ya sayansi inawezekana hakusoma kabisaaa lakini kwenye maisha ya Wizi amefaulu sana amekuwa Profesa bingwa na Mhandisi ktk SOMO LA SAYANSI NA FIZIKIA KWA KUFIKIA KUIBA GESI!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2014

    Si mchezo!

    Watu wanapotoka majumbani kwenda kazini wanaheshimiwa sana kumbe wakifika kazini kazi ni wizi tu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 17, 2014

    watu wa majukumu makubwa majumbani huku kipato kikiwa kiduchu, wanafikia kulazimisha kuyatimiza malengo na majukumu kwa wizi wa gesi kazini!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 17, 2014

    Mbongo akichekewa ana akili sana za wizi, anaweza kuiba hadi kivuli chako!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 17, 2014

    Ebwana eee kumbe wana sayansi tunao?

    Hii ya kuining'iniza Mitungi juu chini chini juu kali!, nadhani hata huko Norway kwenye maendeleo ya gesi hawajawe kui gundua!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 17, 2014

    Hahahahah Mdau wa 4,

    Jamaa walikuwa weupee wakipata Maksi kama namba za viatu zisizo zidi 12% kwenye somo gumu la Physics Sheleni!, lakini kutokana na ukali na kasi ya maisha mtaani wamegeuka kuwa Maprofesa Bingwa wa Physics na Gesi!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 17, 2014

    Kukifikia kiwango kikubwa cha Ufisadi wa Mabilioni ya Fedha, watu wanaanzia ngazi 3 za chini kama hizi:

    1.Wizi wa kwenye mitungi ya gesi
    2.Kukatisha ugawaji wa maji safi DAWASCO, kama yule bingwa wa Kimara Mwisho alivyoweza kuwa Dawasco kwa kugawa maji yeye badalaya Mamlaka yenyewe.
    3.Nauli za ziada kuzunguka na mabasi hadi kituo cha mwisho, mfano unatokea Kimara Bahama mama unageuka na basi hadi Kimara mwisho ili kuelekea Posta, ukitokea Banana Ukonga unageuka na basi hadi Gongo la Mboto ili kwenda mjini Mnazi mmoja !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...