Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa jimbo la Urambo,katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwananchi Skwea mjini Urambo,mkoani Tabora.
Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye yuko katika ziara ya mikoa mitatu ya Tabora,Singida na Manyara,ya kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi mbalimbali ya maenedeleo inayotekelezwa na kusimamiwa na Serikali ya CCM,na pia kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi.
Katika mkutano huo wa hadhara uliowakutanisha Wana Urambo kwa wingi,Kinana pia alisimikwa Uchifu wa kabila la Wanyamwezi.Kubwa zaidi Kinana pia alikabidhi piki piki 16 na baiskeli 95 kwa ajili ya watendaji wa chama cha CCM katika kata na matawi,zilizotolewa na Wabunge Mh,Samwel Sitta wa jimbo la Urambo Mashariki na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora,Mh.Magreth Sitta.
Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Urambo wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Mwananchi Skwea,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara,uliofanyika Wilayani Urambo,Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye yuko mkoani Tabora kwa ziara ya siku 11,za kuimarisha uhai wa chama,kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya CCM,na kusikiliza matatizo mbalimbali ya wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi moja ya piki piki 16 kwa mmoja wa makatibu wa Kata,Bwa.Baraka ambazo zilizotolewa na Wabunge Mh,Samwel Sitta wa jimbo la Urambo Mashariki na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora,Mh.Magreth Sitta.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi baiskeli kwa mmoja wa viongozi wa chama hicho,Bi Fatma Ulaya mjini Urambo katika mkutano wa hadhara.

Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye akiwahutubia Wananchi wa Mji wa Urambo kwenye uwanja wa Mwananchi Skwea
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameketishwa kwenye Kigoda akifanyiwa tambiko mara baada ya kusimikwa Uchifu wa kabila la Wanyamwezi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman akikabidhiwa silaha ya jadi Mkuki,na mmoja wa wazee wa Kinyamwezi mara baada ya kusimikwa Uchifu wa kabila hilo mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Urambo.PICHA NA MICHUZIJR-URAMBO TABORA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...