Kishoka aliyekamatwa Mlimani City. |
TAPELI linalotuhumuwa kukubuhu kwa masuala ya kulaghai watu kwa njia ya kujifanya mfanyakazi wa shirika la Umeme Nchini, Tanesco, jana asubuhi limedakwa baada ya kuwekewa mtego walipokuwa wakitaka kutapeli kwa mmoja wa Afisa wa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma- Ledama.
Kwa mujibu wa Bi. Usia, tapeli huyo alifika asubuhi akiwa na wenzake sita, nyumbani kwake. Wakasema wanatoka Tanesco na hapo wamekuja kucheki mita ya Luku. Baada ya kukorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata Umeme na kung'oa mita, Eti waliona kwenye GPS yao kuwaUmeme hauendi vema.
“Wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! Ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia fasta. Nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umeme wa laki 3 kwa mwezi? Si ingepaswa tulipe kidogo? Wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba Umeme) huwa kinafyatuka halafu Umeme unakwenda zaidi! “ alielezea Bi. Usia, na kuongeza kuwa vishoka hao wakakata Umeme wakaondoka.
"Baada ya kujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halafu wanalazimisha mambo. Wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwa hiyo havisomeki".
"Tukapiga simu Tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka tuite Polisi. Basi tukawapigia simu hao matapeli waje wachukue laki tano waturudishie Umeme, mengine Jumatatu. Wakaja fasta wakarudisha Umeme. Nikawaambia naenda ATM wasubiri. Nikawaacha na mzee nikatoka mbio mpaka Polisi kituo cha Chuo Kikuu nikawahadithia wakanipa Polisi watatu, nikaja nao nyumbani, tukawakuta jamaa wameondoka.
"Mzee akawapigia simu waje hela imepatikana wakasema tukutane Mlimani City. Tukaenda huko, tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia. Tumemuacha selo. Tukaandikisha maelezo. Tunasubiri hatua itakayofuata..."
Hapa likiwa chini ya ulinzi na pingu mkononi.
Mjini hapa hatari sana. Asamilia 80% ya watu waoishia hapa hawana kazi. Kazi zao ndio hizi, utapeli na madili ya kuzuga. Huyu jamaa ana familia yake na baba nayetumainiwa lakini ndio anavyoishi maisha yake kila siku.
ReplyDeletewakipatakana wote wapewe adhabu kali ikiwezekana kifungo cha maisha na picha zao zisambazwe kila mahali ili wajulikane kabisaa. Hawa vishoka wanalipotezea taifa kipato na kuwadhulumu wananchi kwa urohoo wao wa kutaka pesa bila jasho.
ReplyDeleteKuwafunga maisha itakuwa ngumu, kama mdau hapo juu aliyesema asilimia 80% watu ndio wavyoishi hapa mjini. Tatizo ni ajira na mfumo tuliona nao watu wana tamaa. Hawa watu ni talented badala ya kutmia talents zao wanataka hela za haraka haraka na mkato bila kufanya kazi. Tuanzishe mfumo ambao utatoa ajira za kujiari zaidi wenyewe badala ya kutegemea kazi za kuajiriwa kwani hii 80% ni kubwa mno. Yaani kati ya watu kumi unawaona mjini nane kati ya hao ni matapeli wapo wapo tu hawana kazi wanangoja wapate dili watapeli maisha yanakwenda.
ReplyDelete