Rais Jakaya Mrisho Kikwete katikati akifurahia kikundi cha Ngoma cha mkoa wa Ruvuma katika sherehe ya uzinduzi wa Daraja la Ruhekei lililopo katika barabara Mbinga –Mbamba bay mkoani Ruvuma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli wa kwanza kulia wakifanya ishara ya kuweka jiwe la msingi na kufungua Daraja la Ruhekei linalounganisha kati ya Mbinga na Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua Daraja la Ruhekei lililopo katika Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Salma Kikwete pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakipita juu ya Daraja la Mto Ruhekei baada ya kulifungua mkoani Ruvuma. Daraja hilo ni kiungo muhimu kati ya Wilaya mpya ya Nyasa pamoja na Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) kushoto akizungumza na Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu Profesa Juma Athumani Kapuya (Mb) kabla ya uzinduzi wa Daraja la Ruhekei lililopo katika Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) katikati akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe wakati wakisubiri kuwasili kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt.Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya ufunguzi wa Daraja la Mto Ruhekei mkoani Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2014

    Madaraja na Miundombinu nidyo hayo tunaweka sasa ili tusihujumiwe kwa nini tusiweke angalau Kambi za Majeshi na vifaa vya kutosha???

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2014

    Tanzania nyudo ya chuma!

    Me. Raisi Kikwete na Mhe. Membe mpelekeeni taarifa hizi za kukamilika ''DARAJA KATIKA WILAYA MPYA YA NYASA'' zimfikie Raisi wa zamani wa Malawi Joyce Banda!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2014

    This is The United Republic of Tanzania and their incumbent President Hon. Jakaya Kikwete!!!

    Tell this news our neighboring countries Rwanda and Malawi!

    ReplyDelete
  4. Tunakupenda Rais wetu na tunathamini jitihada zako za maisha bora kwa kila mtanzania. Mwenye macho haambiwi tazama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...