Zile habari zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuonesha kwamba hotel ya Naura Spring ya jijini Arusha inawaka moto zilikuwa si za kweli ni watu wametengeza picha hizo ambazo zilikuwa zimeenea kila pembe.
Kamanda wa Polisi Arusha Liberatus Sabas ameongea jioni hii na vyombo vya habari na kukanusha habari za hotel hiyo ya kitalii jijini Arusha kwamba iliwaka moto hizo ni picha za kutengeneza hotel ipo salama kabisa kama unavyoona kwenye picha ya juu. Picha ya chini yake ndiyo iliyosambazwa na watu wasiojulikana.
Wananchi wengi wamepiga simu dawati la usiku la Globu ya Jamii na kueleza masikitiko yao kwa mchezo huu unaoenea kwa kasi nchini hivi sasa. Wamevitaka vyombo husika sio tu kudhibiti uhalifu huu bali pia kuwachukulia hatua watakaobainika kuhusika nao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas ambaye amekanusha kwamba Naura Springs Hotel imewaka moto.
Mambo gani haya ya kuzusha habari ambazo hazikutokea???
ReplyDelete