Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe (kushoto), akipokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Chiola, Wilaya ya Nachingwea
mkoani Lindi baada ya Mwenge huo kumaliza kukimbizwa katika Wilaya Ruangwa. Mwenge huo
wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi,
Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea
ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe (kushoto), akisalimiana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel
Kassanda baada ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru uliotoka Wilaya ya Ruangwa na kuingia
Wilaya ya Nachingwea. Wapili Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo
ambaye ndio aliyekabidhiwa rasmi Mwenge huo kutoka Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda (kulia) akizungumza na wananchi
wa Kijiji cha Chiola (hawapo pichani) baada ya kufungua Mradi wa Nyumba ya Mganga katika
Kijiji hicho kilichopo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe. Mwenge huo
wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi,
Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea
ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda (aliyebeba ndoo ya maji)
akishangiliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina
Chonjo pamoja na wananchi baada ya kubeba ndoo ya maji baada ya kufungua mradi wa
maji katika Kijiji cha Mituguru, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Wapili kulia ni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe
akiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo. Mwenge wa Uhuru ambao mwaka huu 2014
umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate
Katiba mpya” umengia katika wilaya hiyo ambapo unatarajiwa kufungua na kuzindua miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda akizungumza na wananchi wa Kijiji
cha Ikungu, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi baada ya kukabidhi Bajaj kwa walemavu na
Pikipiki kwa watendaji wa Wilaya na Kata mbalimbali katika wilaaya hiyo zikiwa ni kwa shughuli
za maendeleo katika Halmashauri hiyo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe. Mwenge huo wa Uhuru ambao
mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga
Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi
mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe (kushoto), akiwasalimia wapiga kura wake wa Kijiji cha Ikungu wakati wa ukimbizaji
wa Mwenge wa Uhuru katika Jimbo lake la Nachingwea. Waziri Chikawe alimshukuru Kiongozi
wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda pamoja na timu yake kwa kuzindua na
kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake. Picha na zote na Felix Mwagara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...