Na Andrew Chale
TAASISI ya Mwangaza wa buradani Zanzibar (Zanzibar Light Entertainment ) ya mjini Unguja, Zanzibar, Imemtangaza rasmi Hotel ya Kendwa Rocks kuwa eneo litakapofanyika michuano m aalum ya soka la ufukweni lijulikanayo kama (Zanzibar Beach Soccer Championship Bonanza) linalotarajiwa kufanyika Agosti Mbili mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa yao hiyo kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Mwandaaji wa michezo hiyo, Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ ilieleza kuwa, kamati ya mashindano hayo, ambayo kwa sasa hipo katika harakati mbalimbali zikiwemo za kusaka ufadhili kwa wadau, tayari baadhi ya wadau wameanza kuitikia wito huo huku Kendwa Rocks Hotel Beach, wakijitosa kudhamini ‘venue’.
“Kadri siku zinavyozidi kwenda ndipo maandalizi yanakuwa magumu zaidi. Tunafuraha kutoa taarifah kuwa ndipo tutakapofanyia mashindano haya ya Zanzibar Beach Soccer Bonanza 2014.” Alisema Muslim Nassor Jazziphaa.
Aidha, Muslim Nassor Jazziphaa aliweka bayaana kuwa, Director wa Kendwa rocks, Bwana Ally Kilupi tayari ametoa baraka zote za kufaanyika mchezo huo huku akifurahia mchezo kufanyika eneo hilo, huku akitoa rai kuwapo kwa amani na utulivu siku hiyo na siyo kuanza ugomvi na vitu ambavyo havina maana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...