Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi
wa Mahakama, amewateua wafuatao kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania
kuanzia tarehe 13 Agosti, 2014.
WATUMISHI WA MAHAKAMA
(i)
Bw. Penterine Muliisa
KENTE, ambaye
kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani, Dar es Salaam .
(ii)
Bw. Benedict Bartholomew
MWINGWA,
ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam .
(iii)
Bw. Edson James
MKASIMONGWA, ambaye
kabla ya uteuzi alikuwa Katibu wa Jaji Mkuu.
(iv)
Bw. David Eliad MRANGO, ambaye kabla ya uteuzi
alikuwa Msajili, Baraza la Ushindani, Dar
es Salaam .
(v)
Bw. Mohamed Rashid GWAE, ambaye kabla ya uteuzi
alikuwa Msajili, Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi, Dar es Salaam .
(vi)
Dkt. John Eudes RUHANGISA, ambaye kabla ya uteuzi
alikuwa Msajili, Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha.
(vii)
Bw. Firmin Nyanda
MATOGORO,
ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa Naibu Mwenyekiti, Baraza la Rufaa la Kodi, Dar es Salaam .
MAWAKILI WA SERIKALI NA TAASISI MBALIMBALI ZA SERIKALI
(i)
Dkt. Eliezer Mbuki
FELESHI,
ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa Mashitaka, Dar es Salaam .
(ii)
Bi. Barke Mbaraka Aboud
SEHEL, ambaye
kabla ya uteuzi alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Dar es Salaam .
(iii)
Bi. Winfrida Beatrice
KOROSSO ambaye
kabla ya uteuzi alikuwa Katibu Mtendaji, Tume ya Kurekebisha Sheria, Dar es Salaam .
(iv)
Bi. Lilian Leonard
MASHAKA,
ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa, (TAKUKURU), Dar es Salaam .
(v)
Bi. Leila Edith MGONYA, ambaye kabla ya uteuzi alikuwa
Msaidizi wa Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam .
(vi)
Bw. Awadhi MOHAMED, ambaye kabla ya uteuzi
alikuwa Mchunguzi Mkuu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (TAKURURU), Dar es Salaam .
MAWAKILI WA KUJITEGEMEA
(i)
Bw. Lugano J.S. MWANDAMBO, kutoka REX Attorneys, Dar es Salaam .
(ii)
Bw. Amour Said KHAMIS, kutoka AKSA Attorneys, Dar es Salaam .
(iii)
Dkt. Paul KIHWELU, ambaye kabla ya uteuzi
alikuwa Wakili wa Kujitegemeana na Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu Huria, Dar es Salaam .
(iv)
Bi. Rose Ally EBRAHIMU, ambaye kabla ya uteuzi
alikuwa Wakili wa Kujitegemea, Bulyankulu Gold Mine Ltd, Shinyanga.
(v)
Bi. Salma MAGHIMBI, ambaye kabla ya uteuzi
alikuwa Mjumbe, Tume ya Ushindani, (FCC), Dar es Salaam.
WATUMISHI WA VYUO VIKUU
(i)
Dkt. Mary Caroline LEVIRA, ambaye kabla ya uteuzi
alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha.
(ii)
Dkt. Modesta Opiyo
MAKOPOLO,
ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu, Mzumbe,
Morogoro.
Wateuliwa
wote wataapisha tarehe 15 Agosti, 2014 Saa 05.00 asubuhi katika Viwanja vya
Ikulu Dar es Salaam .
Imetolewa na
Mkurugenzi Idara ya habari Maelezo
13 Agosti, 2014
Hongera mama yangu na mwalimu wangu Dkt Modesta Opiyo MAKOPOLO.
ReplyDeleteHongera win Korosso. ruhamgisa na feleshi
ReplyDeleteMabruk Dada yangu Rose sana, nimefurahi sanaaaa ALLAh akujaalie uadilifu, weledi na kila la kheri katika kazi yako hii mpya, iwe ya manufaa kwako, kwa wazazi wako na sisi ndugu zako ...
ReplyDeleteNduguyo mpenzi wa Mtaa wa MSimbazi
MHESHIMIWA RAIS HONGERA KWA UTEUZI WA MAJAJI, ILA NAKUOMBA KAMA UNA UTEUZI MWINGINE KABLA YA MUDA WAKO NAOMBA UTOE KIPAUMBELE ZAIDI NDANI YA IDARA YA MAHAKAMA KULIKO HAO WATU WENGINE UNAOWATEUA ILI WAKAANZE KUJIFUNZA UPYA KUHUSU JUDICIARY NA WAKATI KUNA WATU WALIOFANYA KAZI ZA UHAKIMU KWA MAZINGIRA MAGUMU NA SHIDA NYINGI WAKITEGEMEA SIKU MOJA WATAKUWA MAJAJI, INAKATISHA TAMAA SANA. Mfano huyo wa kutoka Gold mine Bulyankuru to Judge???? jamani inkatisha tamaa sana kwa watumishi wa Judiciary. kwanza hata Gender haikuzingatiwa kwa watumishi wa Judiciary, ina maana hakuna wanawake huko?.....
ReplyDeleteHongera sana!
ReplyDeleteHongereni sana walimu wangu Dr. Levira na Dr. Opiyo I always admired you. Mungu awatangulie katika kazi mpya.
ReplyDeleteKaribuni ili kusaidia kupunnguza kesi!
ReplyDeleteHongera Sana mhadhiri wangu wa Legal Ethics, Prof. Ruhangisa J. Mungu awatangulie katika kusimamia HAKI.
ReplyDelete